Waliotumbuliwa Ubunge na Lipumba CUF Wafungua Kesi Mahakamani
Siku chache baada ya Mwenyekiti wa
Chama cha Wananchi CUF, Prof. Lipumba kuwavua uanachama Wabunge wanane wa Viti
Maalum kisha Spika Ndugai kuridhia uamuzi huo, jana July 27, 2017 Wabunge hao
wamefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Tanzania.
Wabunge hao wamefungua kesi hiyo
iliyopewa namba 143/2017 kupitia Wakili wao Peter Kibatala lakini hata hivyo
bado haijapangiwa Jaji huku Wabunge hao wakidai hawajapewa muda wa kujitetea.
Mbali na kufungua kesi katika
Mahakama Kuu Tanzania, pia wamekata rufaa ndani ya Chama chao kupinga
utekelezaji huo na kuiomba Mahakama isitishe utekelezaji wa uamuzi wa kufukuzwa
Uanachama wao.
No comments