MHE LOWASSA AMLILIA WAZIRI WA USALAMA KENYA
Waziri Mkuu wa
zamani, Edward Lowassa ametuma salamu la rambirambi kufuatia kifo cha Waziri wa
usalama wa Kenya, Meja mstaafu Joseph Nkaissery aliyefariki ghafla katika
hospitali ya Karen iliyopo Nairobi muda mfupi baada ya kupelekwa kwa uchunguzi.
Meja Joseph
Nkaissery alipelekwa hospitali kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla
ya umauti kumkuta, Mkuu wa Utumishi wa Umma wa Kenya Joseph Kinyua
amethibitisha kutokea kwa kifo cha Waziri wa Ulinzi wa Kenya.
Baada ya taarifa
hizo kusambaa Waziri Mstaafu Edward Lowassa amesema Nkaissery alikuwa ni rafiki
mzuri na kiongozi mzuri na wakupigiwa mfano
"Natuma salamu
zangu za pole kwa familia na watu wa Kenya kwa kumpoteza Waziri Joseph
Nkaissery, alikuwa ni rafiki mzuri na kiongozi mzuri wa kupigiwa mfano, Mungu
amumlaze mahali pema peponi" alisema Lowassa
Joseph Kasaine Ole
Nkaissery alikuwa ni mwanasiasa wa Kenya, Mbunge kutoka mwaka 2002 mpaka 2014
na baadaye aliteuliwa kuwa Waziri wa usalama wa Kenya mpaka kifo chake, mbali
na hilo Nkaissery alikuwa kiongozi Mkuu wa jamii ya Maasai nchini Kenya.
No comments