HIVI NDIVYO VIGEZO VITAKAVYOTUMIKA KUWAPANGIA WANAFUNZI MIKOPO 2017/2018
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imesema hivi
karibuni itatangaza sifa na vigezo vitakavyotumika kuwapangia wanafunzi mikopo
ya elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 unaotarajia kuanza miezi michache
ijayo.
Ufafanuzi
huo umetolewa jana (Ijumaa, Julai 7, 2017) jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi
Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa wakati
akijibu maswali ya baadhi ya wateja waliotembelea Banda la HESLB katika Viwanja
vya Mwalimu Nyerere ambako HESLB inashiriki katika Maonyesho ya 41 ya Kimataifa
ya Biashara.
“Tunakamilisha
mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka ujao wa masomo na tumepanga kabla ya mwisho
wa mwezi huu wa Julai tuwe tumeutangaza na tumefungua mtandao wetu ili waombaji
wenye sifa waombe,” alisema Dk Mwaisobwa.
Dk
Mwaisobwa amewataka waombaji wa mikopo watarajiwa wawe watulivu na kufuatilia
kwa karibu vyombo vya habari na tovuti ya HESLB (www.heslb.go.tz) ambayo huwa
na kiunganishi (link) cha mfumo wa kuombea mkopo.
Awali,
katika maonesho hayo, baadhi ya wananchi wanaotarajia kuomba mikopo ya elimu ya
juu wamepata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali yakiwemo tarehe ambayo Bodi
itaanza kupokea maombi ya mikopo kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Dk Cosmas Mwaisobwa
Maswali
mengine yaliyoulizwa ni kama utaratibu wa udahili kupitia vyuoni moja kwa moja
utaathiri upatikanaji mikopo, wengine walitaka kupata elimu zaidi kuhusu
taratibu za urejeshaji wa mikopo.
Akifafanua
kuhusu maswali hayo, Dkt. Mwaisobwa alisema Sheria iliyoanzisha HESLB, pamoja
na mambo mengine, inamtaka mnufaika kuanza kurejesha mkopo wake miezi 24 baada
ya kuhitimu masomo.
Mkurugenzi
huyo wa HESLB alisema kuwa sheria hiyo inamtaka mwajiri yeyote kuwasilisha kwa
HESLB majina ya waajiriwa wake wote ambao ni wahitimu wa taasisi za elimu ya
juu ndani ya siku 28 baada ya kuwaajiri na Bodi itamjulisha kama ni wanufaika
au hapana pamoja na utaratibu na kiwango cha kumkata mnufaika.
Dk
Mwaisobwa aliwataka wananchi kutembelea banda la HESLB kwa kuwa Bodi ya Mikopo
itaendelea kuonyesha shughuli zake kwenye banda lake lililopo ndani, Banda la
Benjamin Mkapa (Namba 19&20) hadi mwisho wa maonyesho hayo, tarehe 13
Julai, 2017.
No comments