WAZEE WA CHADEMA WALAANI KAULI YA MZEE MWINYI KWAMBA MAGUFULI AWE RAIS WA TANZANIA MILELE
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjK4zjsV7O79RxerMMwCppWEXjs74rnYnfwS3Tj-FYkpDvfwSOFepmOwsQL_wOmFfqfnXpdnRL9u3uXnMHkYdKzFBfec4xTatlgAftM579QBE5Ig9-HNDZrPvRWj0o2N2FUlk2ZUsOhIbHP/s640/1.jpg)
Chadema imelaani vikali kauli ya Rais
wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi aliyesema kuwa kama siyo matakwa ya Katiba
ya nchi, uongozi wa Rais John Magufuli ulipaswa kuendelea kuwapo miaka yote.
Kiongozi huyo wa awamu ya pili ambaye
alikuwa akizungumza kwenye swala ya Eid El Fitri alidai pia laiti ingelikuwa
Katiba iliyopo haikufupisha muda wa uongozi wa urais, amengemshauri Rais
Magufuli awe Rais wa Tanzania wa siku zote.
Akizungumzia kauli hiyo katika makao
makuu ya Chadema yaliyopo Kinondoni, leo (Alhamisi) Katibu Mkuu wa Baraza la
Wazee, Roderick Lutembeka amesema matamshi hayo yanapaswa kukemewa kwa vile
yanaashiria kulipeleka Taifa kuandaa viongozi watakopuuza Katiba ya nchi.
“Sisi wazee wa Chadema kwa kutambua
madhara ya kauli kama hizi tumeamua tusikae kimya kwani kauli hiyo
inakiuka Katiba ya nchi inayoweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko kama
ambavyo imetokea kwa nchi jirani zilizopuuza uvunjifu wa katiba,” amesema.
Amewataka Watanzania kwa ujumla
kujitokeza na kupinga kauli za namna hiyo ambazo alisema zinajaribu kuwaandaa
wananchi kisaikolojia ili kuwa na viongozi watakaopindisha Katiba katika siku
za baadaye.
==>Msikilize hapo chini akiongea
No comments