MHE MBOWE: POLISI MSITUZIBE MIDOMO
Mwanyekiti wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe amelitaka jeshi la polisi nchini kutowafunga
midomo na kusema kitendo cha jeshi hilo kuwafukuza waandishi wa habari wakati
wakifanya kazi yao si sawa.
Freeman Mbowe amesema hayo leo
Alhamisi baada ya jeshi la polisi kuwafukuza waandishi wa habari ambao
walikuwa wakifuatilia tukio la kuwasili kwa Mhe. Edward Lowassa Makao Makuu ya
Polisi ambapo leo alikwenda kuitika wito wa jeshi hilo baada ya juzi kutoa
maelezo na kutakiwa kufika leo tena.
Mhe Edward Lowassa alipata wito
kutoka kwa Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI) kumtaka kufika Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi siku ya Jumanne tarehe 27 kufuatia kauli zake alizozitoa ambazo
zinasemakana kuwa ni uchohezi
Lowassa juzi alifika Makao Makuu ya
Jeshi la Polisi na kutoa maelezo yake kwa muda wa masaa manne, kisha baada ya
hapo alijidhamini mwenyewe na kutakiwa kufika siku ya Alhamisi ya tarehe 29
Julai 2017 ambapo amefika na kuambiwa uchunguzi wa jambo lake haujakamilika
hivyo arudi tena tarehe 13 Julai 2017.
==>Msikilize hapo chini akiongea
No comments