SAMSUNG YADHIDI KUJIDHATITI JUU YA KUPAMBANA NA BIDHAA FEKI.
Meneja bidhaa wa
kampuni ya Samsung Tanzania Bw elias Mushi akizungumza katika mkutano waandishi
wa habari makao makuu ua kampuni hiyo jijini dar es salaam.
Meneja wa Pyramid
consumers ltd Bi kareen Babu akielezea walivyojipanga kufanya kazi pamoja na akiahidi
wateja wasamsung kuwa watafanikisha kufikia soko la Tanzania kwa kiwango cha
juu.
Bi Lailatu Jethwa Retail
manager SAMSUNG akitoa ufafanuzi juu ya stika hizo na serial namba ambazo
zitatumika kama namba za usajili pindi unaponunua bidhaa zao ili uweze
kushiriki katika droo hiyo.
Meneja Uzalishaji wa
kampuni ya Samsung Tanzania Bw Rayton Kwembe akifafanua juu ya stika hizo
zitakavyowasaidia wateja wao kutambua bidhaa bora za kampuni hiyo.
Stika za kutambua
ubora wa bidhaa za Samsung pamoja na wakala wa kuasambaza bidhaa zake
Dar
es salaam
Kampuni
ya vifaa vya teknolojia ya Samsung Tanzania imeanzisha mfumo mpya wa uwekaji
stika mbili katika bidhaa zao kwajili ya utambuzi wa bidhaa halisi ikiwa ni
njia ya kupambana na bidhaa feki hapa nchini.
Akitoa
ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari katika
makao makuu ya kampuni hiyo Jijini Dar es salaam, Meneja bidhaa wa
kampuni hiyo Bw. Elias Mushi alisema stika hizo zitasaidia kutambulisha bidhaa
halisi za kampuni hiyo ikiwa ni njia mojawapo ya kupambana na bidhaa feki.
Alisema
bidhaa feki zimekuwa zikihatarisha maisha ya watumiaji hivyo matumizi ya stika
hizo ni jitihada kampuni hiyo katika kukidhi matakwa ya wateja wa Tanzania na ulimwenguni kwa ujumla.
Aidha
Bw.Mushi alifafanua kuwa kuongezwa kwa alama za stika hizo stika moja itakua ikionyesha
jina la msambazaji na ya pili itakua stika inayotambulisha ubora wa bidhaa
halisi ya Samsung.
Akizungumzia
upatikanaji wa bidhaa zao bw Mushi alisema Samsung imeingia ubia na kampuni ya
Pyramid Consumers ltd, kuwa ndio wasambazaji wao kwa lengo la kurahisisha
upatikanaji wa bidhaa zao nchini nzima.
Kwa
upande wake Meneja bidhaa wa Samsung Bi Lailatu Jethwa alisema kampuni ya
Samsung Tanzania wamezindua kampeni ya “Nunua ,sajili, Na Ushinde “
itayoendeshwa kwa mwezi mmoja ikiwa ni kiunganishi cha kupeleka elimu kwa
wateja wao na kupata uzoefu wa kuzitambua bidhaa halisi ya kampuni hiyo.
Alisema
katika bahati nasibu hiyo ambayo kila siku atatangazwa mshindi 1 ambaye
atajishindia bidhaa bora yenye waranti ya miezi 12 toka samsung kwa muda Wa
mwezi mmoja.
Pia
Bi Lailatu aliongeza kuwa hili kuweza kushiriki shinbano hilo unatakiwa kununua
bidhaa yoyote ya Samsung kisha kujisajili kupitia namba za bidhaa (serial
number) walizonunua kwa kutuma ujumbe mfupi (sms) kwenda 0798 222333.
Nae
mkurugenzi wa kampuni ya Pyramid Consumers ltd, Bi Karem Babu-Selema alisema wateja
wa bidhaa Samsung nchini watapata bidhaa bora kupitia kwa mawakala wao waliopo
nchi nzima.
No comments