MZEE WA UPAKO : KUFA MASIKINI NI UJINGA
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhvgIdTbf_ZnUeKwSiW8EA-MihNj35unYq8QXUES5BNtSNaCdxqYh20jPL8Eup6jYajBxBc5Kb9Y0MmnvPwDxgMprXtg1W8-8xcVD8R6ZY5g2yZz3fHNKghdI-Uz4U9uhQNcht8a4heTWM4/s640/1.jpg)
Mchungaji wa Kanisa la Maombezi
(GRC), Anthony Lusekelo alimaarufu kama 'Mzee wa Upako' amefunguka na kusema
mtu kufa maskini si jambo la kusifiwa hata kidogo kuwa ni uzalendo bali ni
Ufala.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo
alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha UJENZI cha EATV
kinachoruka kila Jumapili.
Mzee wa Upako anasema mtu anapokufa
akiwa ameacha mali za kutosha ni jambo jema kwani familia yake nyuma haiwezi
kupata taabu wala watoto hawawezi kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa
na kitanda tu kwani watoto wake watapata shida na mateso.
"Watu wanamsifu mtu amekufa bila
mali eti alikuwa mwadilifu yaani unakuta mtu amefanya kazi serikalini miaka na
miaka, sijui miaka 35 au 40 anakufa hata kitanda hana.
"Wapo watu wanasema huyu jamaa
alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa
fala umenielewa?, huyu alikuwa fala na hastaili kuwa kielelezo cha msingi
tuhoji mtu kapata mali wapi?
"Ndio jambo la msingi sababu
unaacha watoto duniani unadhani wataishi vipi? Mama anakuwa na nyumba pale
anachota kodi anapeleka watoto shule maisha yanaendelea" alisisitiza Mzee
wa Upako.
No comments