MAALIM SEIF ASHTUKIA MCHEZO MCHAFU ULIOFANYWA NA MSAJILI WA VYAMA NA RITA, KUSAJILI BODI YA LIPUMBA.
Chama
cha wananchi cuf kimeeleza kushtushwa na muendelezo wa hujuma zinazofanywa na
msajili wa vyama vya siasa nchini jaji Fransic Mutungi dhidi ya cuf kwa kutumia
wakala wa usajili (RITA)
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na katibu mkuu wa chama cha wananchi cuf kuwa hujuma hizo zinahusisha
mbinu chafu za kughushi nyaraka ambazo kwa mujibu wa Maalim Seif rejea kikao
kilichofanyika tarehe 9 April 2017 zimesema kuwa lengo la Mutungi ni kumsaidia
Profesa Lipumba kuhakikisha bodi ya wadhamini feki inasajiliwa.
Amesema kuwa bodi hiyo ambayo
iliandaliwa kuchukua nafasi ya bodi halali wadhamini ya cuf kwakuwa chama cha
wananchi ni kikwazo katika kufanikisha mipango yao haramu ya kufungua akaunti
mpya ya benki ili kuwezesha wizi wa ruzuku ya chama.
Aidha maalim Seif amebainisha kuwapo
kwa taarifa kuwa afisa mtendaji mkuu wa RITA amepata shinikizo kubwa la
kusajili wajumbe feki wa bodi ya wadhamini ya cuf kwa kutumia majina
yaliyowasilishwa na pro.Lipumba ili kuhujumu majina halali yaliyopitishwa na
baraza kuu la uongozi la Taifa ya kikao kilichofanyika tarehe 19 march huko
Zanzibar.
Ameongeza kusema kitendo cha RITA
kukataa kumpa nafasi maalim Seif ambaye aliandika barua tatu machi 31 na june 6
2017 ya kukutana na kabidhi wasihi mkuu wa RITA na wakati huo ikimpa
nafasi Lipumba kimedhihirisha kuwa RITA wamejiunga na jaji mutungi jambo ambalo
limepelekea cuf kuadhimia kufungua kesi dhidi ya RITA kwa kukiuka sheria.
Chama cha cuf kimewakutanisha wabunge
40, madiwani pamoja na wanachama ili kutoa taarifa kwa umma dhidi ya maadhimio
ya kusimamisha kesi nyingine zote hadi shauri linalohusu uhalali wa maamuzi ya
RITA litakapoamuliwa.
No comments