Breaking News

MFUMUKO WA BEI WA TAIFA KWA MWEZI MEI, 2017 UMESHUKA HADI ASILIMIA 6.1

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwezi Mei, 2017 umepungua hadi asilimia 6.1 kutoka asilimia 6.4 ilivyokuwa mwezi Aprili, 2017.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, Ephraim Kwesigabo amesema kupungua kwa mfumuko wa bei kunatokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma ikilinganishwa na kasi iliyokuwepo kwa mwezi Aprili, 2017.


No comments