ACACIA YAIBUKA NA KUPINGA VIKALI MATOKEO YA KAMATI YA PILI YA MHE RAIS KUHUSU MCHANGA WA MADINI
Mwitikio wa Acacia kwenye matokeo ya
kamati ya pili ya Rais
Acacia imeona matokeo ya
kushtua ya kamati ya pili ya Rais iliyowasilishwa kwa Rais wa Tanzania Mh. Dk
John P. Magufuli leo asubuhi ambayo imeangalia nyanja za historia za kiuchumi
na kisheria ya mauzo ya nje ya makanikia ya madini.
Kamati ya Pili imetoa matokeo
yake kwa kutumia matokeo ya Kamati ya Rais ya Kwanza, iliyotangazwa tarehe 24
Mei 2017, ambayo Acacia imeikanusha vikali. Kamati hiyo ilipata matokeo yake
kwa kutumia sampuli ya kontena 44.
Kwa mujibu wa data za zaidi ya miaka 20
tulizonazo ni vigumu kuoanisha matokeo yetu na yaliyokutwa na kamati, na kamati
imetoa thamani ya juu kwa zaidi ya mara 10 kuliko thamani halisi ya makanikia
Kamati ya Pili inadai kuwa
Acacia imetangaza kiasi cha chini cha mapato kuliko inavyopata na kulipa kodi
kidogo kuliko inavyostahili kwa miaka mingi na kuficha mabilioni ya dola ya
Marekani. Na hivyo imefanya mapendekezo kadhaa ikiwa ni pamoja na Acacia kulipa
kodi inayodaiwa na mirahaba, kufanya majadiliano upya ya mikataba mikubwa ya
uchimbaji madini, umiliki wa Serikali katika migodi, na muendelezo wa marufuku
ya kuuza nje.
Acacia inakanusha vikali
tuhuma hizi mpya zisizo na ushahidi. Sisi tumefanya biashara zetu kwa utaratibu
bora kabisa na kwa kufuata sheria zote za Tanzania. Tunarudia kusema tena
tumeweka wazi kila kitu chenye faida tulichokuwa tunazalisha tangia tuanze
uchimbaji Tanzania na tumelipa kodi na mirabaha yote inayotakiwa kulipwa, na
kwa kuongezea mahesabu yetu tunayotoa yanakaguliwa kila mwaka kwa viwango vya
kimataifa vinavyoendana na IFRS.
Acacia kwa muda mrefu tulitaka
kushirikiana na Serikali ya Tanzania kwa kuwa tunaamini wote tuna malengo sawa
katika kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini. Hata hivyo,
ushirikiano huu lazima uwe na misingi ya haki kwa wadau wote, ikiwa ni pamoja
na 96% ya wafanyakazi katika migodi yetu ambao ni Watanzania, na wanahisa wetu
ambao wamechangia dola bilioni 4 za uwekezaji ambazo Acacia imefanya ndani ya
nchi hadi sasa.
Acacia bado inakaribisha
mazungumzo na Serikali kuhusu suala hili na inaendelea kutathmini nini inaweza
kufanya . Tutatoa taarifa zaidi kwa soko kadri tutakavyoweza kufanya .
No comments