ZITTO KABWE AMEANDIKA HAYA KUFATIA KURIPOTIWA ZA KUJIUZULU MSHAURI WA ACT WAZALENDO ALBERT MSANDO
Nimepokea barua ya
Wakili Albert G. Msando kuomba kujiuzulu nafasi yake ya Ushauri wa Chama chetu
cha ACT Wazalendo.
Ndugu Msando
anawajibika Kwani anapaswa, nanukuu kutoka katika barua yake, "kuishi Kama
mfano Kwa jamii inayonizunguka".
Ndugu Albert Msando
amekuwa kiongozi mwenye mchango mkubwa katika chama katika nafasi mbalimbali
alizoshika ndani ya chama. Chama kinamshukuru kwa moyo wake wa kuzalendo na
mchango alioutoa katika Chama. Ni matumaini yetu ataendelea kushirikiana nasi
katika ujenzi wa chama kwa kadri atakavyoweza na atakapohitajika kama
mwanachama.
Nikiwa Kiongozi wa
Chama nimekubali kuwajibika kwake na kumtakia kheri katika kujisahihisha kwake.
Ndugu Msando Alberto
ameomba msamaha Kwa jamii kwa uwazi na ni wajibu wetu kumsaidia kupita katika
mitihani iliyomkumba.
Kabwe Z. Ruyagwa
Zitto
Kiongozi wa Chama -
ACT Wazalendo
Dar es salaam
Mei 23, 2017