WAFANYA BIASHARA SASA KUOGA NEEMA BAADA YA RAIS MAGUFULI KUTOA TUMAINI JIPYA

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli jana tarehe 06
Mei, 2017 alizindua Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuongoza Mkutano wa
10 wa Baraza hilo uliofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baraza
hili ni la tatu na mkutano huu ni wa kwanza kuongozwa na Mhe. Rais Magufuli
tangu aingie madarakani ambapo tofauti na mikutano mingine, Mhe. Rais Magufuli
aliendesha majadiliano ya pamoja ambapo wajumbe wa baraza na wawakilishi
wengine kutoka sekta binafsi walipata fursa ya kutoa maoni, mapendekezo na
dukuduku, kisha kupatiwa majibu kutoka kwa Mawaziri, Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa Majaliwa na Mhe. Rais.
Miongoni
mwa yaliyojitokeza ni kuiomba Serikali kuendelea kushirikiana na sekta binafsi
katika upangaji na utekelezaji wa mipango, sera na sheria mbalimbali za
uwekezaji na biashara, kuendelea kuondoa vikwazo na urasimu ambao unachangia
kupunguza ufanisi katika biashara na uwekezaji, kuongeza vivutio vya uwekezaji
na kuendelea kushirikisha sekta binafsi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali
ya maendeleo ikiwemo ujenzi, utalii na viwanda.
Aidha,
wawakilishi wa sekta binafsi waliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano kwa juhudi
kubwa inazozifanya kujenga miundombinu muhimu kwa uwekezajina biashara kama
vile ujenzi wa reli, barabara, meli na ununuzi wa ndege, kukabiliana na rushwa,
kusimamia mpango wa ujenzi wa viwanda, kujenga nidhamu na uwajibikaji wa
watumishi wa umma na kujenga uhusiano mzuri na mataifa mbalimbali duniani.
Pamoja
na majibu yaliyotolewa na Mawaziri ambao ni wajumbe wa Baraza la Taifa la
Biashara, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewaahidi wawakilishi wa sekta
binafsi waliohudhuria mkutano huo kuwa Serikali itahakikisha maoni yao yote
yanafanyiwa kazi ili Taifa liweze kunufaika na rasilimali zake na kusonga mbele
kimaendeleo.
“Naomba
niwahakikishie kuwa hisia zenu tumezipata, maoni yenu tutayazingatia na
tutahakikisha tunayafanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kwa pamoja tufanye kazi
ya kuijenga nchi yetu” alisema Mhe. Majaliwa.
Mhe.
Rais Magufuli aliwapongeza wajumbe wa Baraza la Taifa la Biashara pamoja na
Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) inayoongozwa na Mwenyekiti wake Dkt.
Reginald Mengi kwa juhudi kubwa zinafanywa kuendeleza biashara na uwekezaji
nchini na amewaahidi kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendelea kuwathamini na
kushirikiana na wawekezaji na wafanyabiashara kwa manufaa ya Taifa.
Mhe.
Rais Magufuli alielezea kufurahishwa na maoni, mapendekezo na dukuduku
alizozipata kutoka kwenye mkutano huo na amewakikishia kuwa Serikali anayoiongoza
itafanyia kazi maoni yote yaliyotolewa ikiwemo kuondoa usumbufu unaosababishwa
na uwingi wa taasisi zinazomhudumia na kumtoza mfanyabiashara na mwekezaji,
kuongeza vivutio, kuboresha mifumo ya ukusanyaji wa kodi mbalimbali na
kuishirikisha sekta binafsi katika mipango na utekelezaji wa miradi.
Kuhusu
tatizo la ucheleweshaji wa mizigo bandarini Mhe. Rais Magufuli aliagiza kuanzia
Jumatatu tarehe 08 Mei, 2017 taasisi zote zinazotoa huduma katika bandari ya
Dar es Salaam ziungane na Mamlaka ya usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kutoa
huduma kwa muda wote wa saa 24.
“Kama
alivyosema Waziri Mkuu, tunataka kufanyia kazi maoni yenu mara moja, kuanzia
Jumatatu nataka taasisi zote za pale bandarini zitoe huduma saa 24, haiwezekani
bandarini kwetu mizigo ichukue siku 13 kuitoa bandarini wakati bandari za
wenzetu majirani inatoka baada ya siku 3, tutashindana vipi?” alihoji Mhe. Rais
Magufuli.
Hata
hivyo Mhe. Dkt. Magufuli aliwataka wafanyabiashara na wawekezaji wajirekebisha
kwa kasoro ambazo baadhi yao wanazo ikiwemo ukwepaji wa kodi, kupandisha
viwango vya bei kwa huduma wanazotoa Serikalini, kujihusisha na rushwa, kutaka
faida kubwa isiyostahili bila kuwajali wananchi na kutochangamkia fursa za
uwekezaji za ndani na nje ya nchi licha ya juhudi zake za kuwaleta viongozi na
wafanyabiashara kutoka nchi mbalimbali.
“Nataka
mjiulize amekuja Waziri Mkuu wa India, amekuja Rais wa Vietnam, amekuja Rais wa
Uturuki, amekuja Rais wa Kongo (DRC), amekuja Rais wa Zambia, amekuja Rais wa
Uganda, amekujaMfalme wa Morocco na wengine wengi, tumenufaikaje? Mbona wao
wanakuja kuwekeza hapa nyie kwa nini hamuendi kwao?” alihoji Mhe. Rais
Magufuli.
Gerson
Msigwa
Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar
es Salaam
No comments