Breaking News

SHEIKH JALALA: VIJANA TUTUMIE DINI ZETU KUDUMISHA AMANI, UMOJA, UTULIVU NA UPENDO ULIOPO NCHINI


Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh Hemed Jalala akizngumza na wanahabari mara baada ufunguzi wa semina, Katika ukumbi wa Nkuruma chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)
Mtoa mada katika semina hiyo Dr Josephat Muhoza ambaye ni Mtaalamu wa Falsafa Kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salam akizungumza na Wanahabari  nje ya ukumbi wa Nkuruma, chuo kikuu cha dar es salaam.


Washiriki wa semina hiyo wakitatilia kwa umakini mada zinazowasilishwa

Dar es salaam
Vijana nchini Tanzania wametakiwa kuendelea  kutumia dini zao kama viungo vya kudumisha Amani, utulivu, na upendo  uliopo sasa nchini badala ya kutumia dini zao kutengeneza migogoro na mifarakano katika jamii jambo ambalo lina madhara makubwa katika ustawi wa taifa.

Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam Kiongozi Mkuu wa kiroho wa waislam wa dhehebu la Shia ITHNASHERIYA Tanzania Sheikh Hemed Jalala mara baada ya ufunguzi wa semina maalum iliyofanyika  Ukumbi wa Nkuruma (UDSM) chuo kikuu cha Dar es salaam katika ambayo imewakutanisha wasomi, wanazuoni na vijana kujadili namna ya kumuunganisha Mwanadamu na dini yake, sambamba na kutambua Tunu zilizopo katika dini yake.

Alisema kwa sasa dunia ipo hatarini na inakabiliwa na wimbi la kuweza kuibuka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambavyo katika nchi nyingi dini ndio kimekuwa kichocheo kikubwa cha migogoro jambo ambalo alisema limepelekea wao kuandaa semina hii kwa lengo la kuwakutanisha Vijana Pamoja na wataalam mbalimbali kuwakumbusha namna bora ya kuitumia dini yao kulinda Amani na kuepuka migogoro.

“Tanzania inasifa ya Amani, upendo, utulivu, kuheshimiana, kutokubaguana, hivyo vijana tunahitajika kuhakikisha kuwa tunaenzi Tunu hizi kwa hali na mali ili tuendelee kuwa na sifa ya kisiwa cha Amani duniani”alisema Kiongozi huyo wa Dhehebu la Shia nchini.

Kwa upande wake Mwanafalsafa wa kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam Dr Josephat Muhoza akizumza mara baada ya ukizungumza katika semina hiyo amewataka watanzania kutanguliza Ubinadamu mbele na kisha dini zao baadae kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wamejiepusha na migogoro kama inayoshuhudiwa katika mataifa mengineyo duniani.

No comments