AGA KHAN KUFANYA UPASUAJI KWA WHATSAPP

Dar
es Salaam.
Madaktari
wa Hospitali ya Aga Khan na Prince Aly Khan nchini India, wanatarajia kuboresha
huduma za upasuaji wa mifupa na majeraha kwa kutumia mtandao wa What’sApp.
Teknolojia
hiyo mpya inatarajiwa kuanza kutumika nchini baada ya madaktari bingwa kutoka
India kuwasili. Madaktari hao kutoka Hospitali ya Prince Aly Khan waliwasili
nchini jana kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wenzao wa Hospitali ya Aga Khan
kutumia teknolojia hiyo ya kisasa kufanya upasuaji.
Daktari
bingwa wa upasuaji mifupa na majeraha wa Hospitali ya Aga Khan, Harry Matoyo
amesema madaktari hao walioanza upasuaji wataondoka Jumatatu na kwamba,
wanatarajia wataalamu wa hospitali hiyo watakuwa wamenufaika na uzoefu
watakaopata.
“Tumetengeneza
group (kundi) la What’sApp ambalo litatumiwa na madaktari bingwa wa upasuaji
mifupa kati ya nchi hizi mbili, kwa ajili ya kusaidiana iwapo tutakwama wakati
wa upasuaji. Tunaweza kupiga picha na kuuliza kitu kinachotakiwa kufanyika,”
alisema Dk Matoyo.
source mawingu blog
No comments