WASICHANA 82 WALIOTEKWA MWAKA 2014 , WAACHIWA HURU NA BOKO HARAM

Ofisi
kuu ya Rais wa Nigeria imethibitisha kuwa wanafunzi 82 wa shule ya wasichana wa
Chibok, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram mnamo mwaka wa
2014, wameachiwa huru.
Maafisa
wanasema kuwa waliachiwa huru, kufuatia majadiliano ya muda mrefu na
ubadilishanaji washukiwa wa Boko Haram, waliokuwa wamezuiliwa na wakuu wa nchi
hiyo.
Wasichana
hao ni miongoni mwa zaidi ya wanafunzi wanafunzi 270 waliotekwa nyara kutoka
shule ya malazi katika mji wa Chibok ulioko kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Wasichana
hao wote 82 kwa sasa wanalindwa na jeshi la Nigeria mahali salama, baada ya
kuletwa kwa barabara kutoka maeneo ya ndani kabisa vijijini, hadi katika kambi
ya jeshi ya Banki, karibu na mpaka na Cameroon, hayo ni kwa mjibu wa mwaandishi
habari wa BBC Stephanie Hegarty kutoka Lagos.
Mwaandishi
wetu anasema kuwa, familia nyingi huko Chibok wamefurahia taarifa hiyo ya hivi
punde lakini wapiganaji hao wa Boko Haram, wangali wakiwazuilia zaidi ya
wanafunzi 100.
Ni
sehemu ya maelfu ya watu ambao wametekwa nyara na wanamgambo hao, walioanzisha
vuguvugu hilo miaka minane iliyopita.

Utekaji
nyara huo ambao ulifahamika baadaye kama "Chibok girls" ulisababisha
kilio kikubwa kote duniani na kampeini za kutaka waachiwe huru ikatanda kote
katika mitandao ya kijamii.
Kabla
ya hatua hii ya hivi punde ya kuwaachia wasichana hao, inakisiwa kuwa zaidi ya
wasichana 195 wangali hawajulikani waliko.
Idadi
ya washukiwa wa Boko Haram ambao wameachiwa huru na utawala wa Nigeria, bado
haijajulikana.
No comments