WAZIRI MKUU ABARIKI UTARATIBU WA TRA KUSAKA WADAIWA SUGU WA KODI KWA MTUTU WA BUNDUKI
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
ameibariki Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuendelea kuwatumia TAKUKURU pamoja
na Jeshi la Polisi wenye silaha za moto wakati wanapokwenda kukusanya mapato
pamoja na kodi kwa wafanyabiashara ambao ni wanadaiwa sugu.
Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la
Arusha Mjini Godbless Lema katika kipindi cha maswali kwa Waziri Mkuu Bungeni
Mjini Dodoma, amesema ni sahihi kwa kikosi kazi hicho (task force) kutumika kwa
kuwa wapo baadhi ya wafanyabiashara sugu wenye lengo baya la kutotaka kulipa
madeni na badala yake hutoa rushwa.
Mhe. Lema alitaka kusikia kauli ya
serikali juu ya mfumo unaotumiwa TRA wa kusumbua na kuwatisha wafanyabiashara
katika shughuli zao za kila siku huku ikiwa inadaiwa kuwa mamlaka hiyo hutumia
Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa na TAKUKURU katika miji mikubwa ikiwemo Dar
es Salaam, Mwanza , Arusha na Mbeya.
“Ni kweli kwamba tunacho chombo
ambacho kinachowajibika katika ukusanyaji wa mapato na kodi kutoka kwa walipa
kodi wetu wafanyabiashara wakiwemo, lakini TRA kutumia ‘task force’ haina maana
ya kuwatishia amani wafanyabiashara ila lengo lake ni kufuatilia wadaiwa sugu
japokuwa siyo wote ila wachache hawataki kabisa kulipa pamoja na kwamba wanajua
wao ni wadaiwa sugu..... Tunatumia TAKUKURU kwa sababu kuna wengine hutumia
fursa hiyo kutaka kuwahonga maafisa wa TRA ili wafutiwe madeni yao”. Alisema
Majaliwa
Vile vile Majaliwa amesema ‘task
force’ imeundwa na TRA wenyewe ili kuona wanapokwenda kukusanya madeni yao
hakutumiki vitendo ambavyo havikubariki kama vile utoaji wa rushwa ili madeni
hayo yasilipwe au namna nyingine yoyote ambayo mfanyabiashara anaweza kuona si
sahihi kwake
No comments