WAPINZANI WAUNGANA KUMNG'OA MUGABE UCHAGUZI MKUU UJAO
Viongozi wawili wa
vyama vya upinzani nchini Zimbabwe wamekubaliana kuunda umoja kuwania urais
kwenye uchaguzi mkuu ujao nchini humo.
Kiongozi wa Movement
for Democratic, Morgan Tsvangirai na aliyekuwa makamu wa rais wa nchi hiyo
Joice Mujuru wa National people's Party walitia saini makubaliano hayo siku ya
Jumatano.
Rais wa nchi hiyo
Robert Mugabe awali alitoa maneno ya dhihaka kutokana na mipango ya upinzani
aliyodai kuungana kumuondoa madarakani.
Morgan Tsvangirai
na Joice Mujuru wameonekana kumaliza baadhi ya tofauti zao.Tsvangirai anasema
makubaliano yaliyotiwa saini baina ya vyama viwili ni msingi kuelekea kuunda
umoja wa vyama kwa ajili ya kupambana na chama tawala Zanu PF.
Changamoto iliyopo
hivi sasa ni kuamua nani kati ya hao wawili ataongoza muungano huo.
Tayari, vyama vingi
vidogo vya upinzani vimemuidhinisha Morgan Tsvangirai kuwa mgombea wao wa
urais.
Kiongozi wa miaka
mingi madarakani Robert Mugabe , alieleza kuwa upinzani umejaa watu wasio na
kitu vichwani.
Amesema hakosi
usingizi kwa kile kinachoitwa umoja wa wapinzani.
Chanzo: BBC
No comments