TPDC KUSAMBAZA GESI ASILIA KWA KUSHIRIKIANA NA SEKTA BINAFSI
TPDC kwa
kushirikiana na Sekta binafsi wanatarjia kutekeleza miradi mbalimbali ya
usambazaji wa gesi asilian katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara
na baadhi ya mikoa mingine itakayoidhinishwa.
Hayo yamebainishwa
na Kiamu Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC Mhandisi Kapuulya Musomba wakati
akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake jana Jijini Dar es
Salaam.
Mhandisi Musomba
alisema kuwa miradi hiyo imeanza kwa kupitia upya taarifa ya awali ya upembuzi
yakinifu wa mradi wa ujenzi wa mtandao wa bomba la kusambazia gesi asilia
katika Jiji la Dar es Salaam, ambapo mnamo mwezi machi 22, 2017 TPDC
ilikaribisha jumla ya makampuni 9 ambayo yalikidhi vigezo vya kimanunuzi kwa
ajili ya kazi hiyo.
“Napenda kuutaarifu umma kuwa TPDC
inatarajia kutekeleza miradi mbaimbali ya usambazaji wa gesi asilia katika
mikoa ya Dar es Salaam, Bagamoyo na Mkuranga Mkoani Pwani, Lindi na Mtwara
pamoja na baadhi ya mikoa mingine,” alisema
Mhandisi Muyomba.
Aliongeza kuwa
lengo la kupitia upya taarifa za awali ni kuboresha zaidi taarifa za kifedha,
mahitaji ya kiufundi na utambuzi wa njia za kupitisha bomba na ugawaji wa kanda
za usambazaji.
Aidha alisema kuwa
ili kuharakisha usambazaji wa gesi, TPDC inakaribisha na kuhamasisha sekta
binafsi kuwekeza katika uendelezaji wa miundombinu itakayowezesha usambazaji wa
gesi asilia katika Jiji la Dar es Salaam mara tu mapitio ya upembuzi yakinifu
utakapomalizika.
Mtandao huo
unakadiriwa kuwa na urefu wa takribani kilomita 65 ambao utahudumia, kwa
kuanzia, nyumba 30,000, viwanda na vituo vya kushindilia gesi asilia pamoja na
vituo vya kujazia gesi hiyo.
Katika hatua
nyingine Kaimu Mkurugenzi Mtendaji huyo alisema kuwa hadi sasa TPDC imefanikiwa
kukiunganisha na mtandao wa gesi asilia Kiwanda kimoja cha kutengeneza Vigae
cha Goodwill kilichopo Mkuranga, Mkoani Pwani huku likiendelea na majadiliano
na viwanda vingine vitatu kwa ajili ya kuunganishwa na mtandao huo.
Kwa mujibu wa
Sheria ya Mafuta ya Mwaka 2015 TPDC inatambuliwa kuwa Shirika rasmi la taifa
linalojiendesha kibiashara, ambapo sheria hii inaipa mamlaka TPDC kuruhusu
makampuni mbalimbali kuendesha shughuli za sekta, zitakazokuwa zainadhibitiwa
kwa utaratibu maalum chini ya usimamizi wa Mdhibiti anayetoa leseni.
No comments