TAARIFA KWA UMMA: AJALI YA TRENI NA DALADALA YA KUTOKA GONGO LA MBOTO ALFAJRI LEO APRILI 19, 2017.
Mtu mmoja amefariki dunia baada ya
kutokea ajali ya basi la abiria/daladala (T 435 DGG) kutoka Gongo la Mboto
kwenda Mnazi Mmoja kuigonga treni ya Pugu leo Aprili 19, 2017 saa 11 alfajiri
katika makutano ya reli na barabara ya Nkurumah jijini Dar es Salaam.
Majeruhi wa ajali ni 23 , wanane wapo
hospitali ya Amana na waliobakia 15 wapo Hospitali ya Taifa Muhimbili MOI
watatu kati yao ni mahututi. Taarifa zaidi itatolewa kuhusu ajali hiyo.
Hata hivyo treni ya Pugu inaendelea
na huduma zake kwa kufuata ratiba.
Imetolewa na Afisi ya Uhusiano kwa
niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TRL
Nd. Focus Sahani,
Dar es Salaam,
Aprili 19, 2017.
No comments