SAKATA LA WATUMISHI WE VYETI FEKI LACHUKUA SURA MPYA
Sakata la watumishi wa umma kushughi vyeti vya elimu limezidi
kuchukua sura mpya na sasa wamefikia zaidi ya 10,000.
Hatua hiyo, inatokana na uhakiki uliofanywa na Sekretarieti ya
Ajira katika Utumishi wa Umma ambayo imebaini waombaji kazi 39,511 kati yao,
1,951 wana vyeti vya kughushi.
Kuongezeka kwa idadi hiyo, kunatokana na kauli ya Rais Dk. John
Magufuli, wiki iliyopita, kwamba anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali
ambao wamebainika kuwa na vyeti feki.
Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam, wakati akizindua mabweni mapya
ya wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Alisema anafahamu idadi ya watumishi wenye vyeti feki ni zaidi
ya 9,000 na anaisubiri ripoti hiyo kuifanyia kazi.
“Kwa hiyo mnaweza mkaona shida
zilizopo katika nchi hii, huku wafanyakazi hewa karibu 19,000, wanafunzi hewa
ni zaidi ya 56,000, kila mahali unapokwenda ni matatizo, lakini ni lazima
niyatatue matatizo kwa sababu mlinichagua kwa ajili hiyo,” alisema Rais Magufuli.
Akiwasilisha hotuba ya bajeti ya mwaka 2017/18 kwa ofisi yake
jana bungeni mjini hapa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi
wa Umma na Utawala Bora, Angella Kairuki, alisema baada ya kubainika kwa hali
hiyo, wahusika waliondolewa kwenye mchakato, huku vyeti hivyo vikiwasilishwa
katika mamlaka husika kwa hatua za kisheria.
“Wahusika waliondolewa katika
mchakato pamoja na vyeti hivyo kuchukuliwa na kuwasilishwa kwa mamlaka husika
kwa ajili ya hatua zaidi,” alisema
Kairuki.
Hata hivyo, zipo taarifa zinazodai kuwa orodha ya watumishi wa
umma ambao wamebainika kuwa na vyeti feki itawekwa hadharani Aprili 30.
Zaidi inaelezwa kuwa sakata hilo la vyeti feki linawagusa pia
mabalozi ambao ni wawakilishi wa Watanzania katika mataifa mbalimbali, wakuu wa
wilaya na mikoa.
No comments