HUU NDO UWEZO WA KOREA KASKAZINI KIVITA. ANA MAKOMBORA ZAIDI YA 1000 YANAYOWEZA KURUSHWA TOKA BARA MOJA HADI JINGINE
Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye
uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia
Marekani.
Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.
Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.
Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda
makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine
ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.
Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa
marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.
Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho
Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba
2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo
baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.
Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea
Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi
Marekani.
Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo
linalojulikana kama KN-14. Hata hivyo makombora hayo hayajafanyiwa majaribio.
Lakini mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio,
muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa
katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza
kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.
Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini
ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.
Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa
jina Hwasong.
Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi
ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.
Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na
yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.
Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama
Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na
kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.
Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.
Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo
yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran
Ramani ya Korea Kaskazini na majirani zake wa Korea Kusini
Korea Kaskazini ilianza mpango huo mapema miaka ya 80 kutengeza
kombora la masafa ya kadri kwa jina Nodong likiwa na uwezo wa kusafiri urefu wa
kilomita 1000.
Kombora hilo limetengezwa kwa muundo wa Scud, lakini ni asilimia
50 kwa ukubwa na lina mashine yenye uwezo mkubwa.
Uchanganuzi wa mwezi Aprili 2016 wa taassii ya kimataifa kuhusu
utafiti wa mikakati ,unasema kuwa makombora hayo yalithibtishwa yanaweza kupiga
maeneo yote ya Korea Kusini na Japan.
Imeongezea kuwa maonyesho ya Oktoba 2010 yalithibitisha kuwa
kombora hilo linaweza kufika urefu wa kilomita 1,600 ikimaanisha kwamba
linaweza kupiga kambi kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la Okinawa.
Makombora hayo ya Nodong yanadaiwa kujaribiwa 2006, 2009, 2014
na 2016.
Kombora la Musudan
Korea Kaskazni imekuwa ikitengeza makombora ya Musudan kwa miaka
kadhaa, na hivi karibuni ilifanya majaribio 2016.
Makadirio yanatofautiana kuhusu viwango vyake, huku ujasusi wa
Israel ukitaja uwezo wake kuwa kilomita 2,500 nacho kitengo cha ulinzi wa makombora
nchini Marekani kikikadiria kuwa na uwezo wa kufika kilomita 3,200.
Duru nyingine zinasema kuwa kombora hilo lina uwezo wa kwenda
kilomita 4,000.
Kombora la masafa mafupi la Musudan ambalo pia linajulikana kama
Nodong B ama Taepodong-x linaweza kulishambulia taifa lote la Korea Kusini na
Japan.
Kombora hilo linaweza kushambulia kambi za kijeshi za Marekani
katika eneo la Guam.
Kombora la masafa marefu la Taepodong linaloweza kurushwa kutoka
bara moja hadi jingine
Korea Kaskazini inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la
masafa ya kadri, kwa jina Pukguksong, mnamo mwezi Agosti 2016 likirushwa kutoka
kwa manuwari.
Kombora la pili lilirushwa kutoka ardhini mnamo mwezi Februari
2017.
Pyongyang ilisema kuwa ilitumia mafuta ,na kufanya kuwa rahisi
kuliwasilisha na kurusha. Hatahivyo maelezo kuhusu uwezo wake hayajulikani.
Credit: BBC
No comments