RAIS MAGUFULI, MAKOMANDOO KUPAMBA SHEREHE ZA MIAKA 53 YA MUUNGANO DODOMA
Na: Lilian Lundo -
MAELEZO.
Maonesho ya
ukakamavu na mbinu za medani katika kupambana na adui hasa kulinda amani ya
nchi yetu kutoka Kikosi Maalum cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania
(JWTZ), itakuwa ni sehemu ya shamrasha zitakazopamba maadhimisho ya miaka 53 ya
Muungano yatakayofanyika kwa mara ya kwanza mjini Dodoma Aprili 26 mwaka huu.
Kwa mujibu wa
taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira,
Kazi, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama maadhimisho hayo
yanatarajiwa kuhudhuriwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, pia yatapambwa na
burudani nyingine kutoka vikundi mbalimbali.
Taarifa ya Waziri
Mhagama ametaja shughuli nyingine zinazotarajiwa kufanyika siku ya Muungano
kuwa ni gwaride la heshima lililoandaliwa na vikosi vya ulinzi na usalama
(JWTZ,JKT, Polisi na Magereza) na onesho la mbwa na farasi waliofunzwa.
Aidha, Waziri
Mhagama aliongeza kuwa mambo mengine yatakayofanyika ni gwaride la uzalendo la
wanafunzi wa shule za sekondari za Dodoma, burudani za vikundi vya ngoma za asili
kutoka Dodoma na Zanzibar, Yamoto Band, vikundi vya muziki wa kizazi kipya
kutoka kwa wasanii Mchungaji Zayumba, Jacob Beats, Mwenge Jazz Band na Mgosi
Maturumbeta.
“Kauli mbiu ya sherehe za kutimiza
miaka 53 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Miaka 53 ya Muungano;
Tuulinde na Kuumarisha, Tupige Vita Dawa za Kulevya na Kufanya Kazi kwa Bidii,”alifafanua Waziri Jenista Mhagama.
Ametoa wito kwa
wananchi wote nchini kusherehekea siku hiyo muhimu kwa kudumisha amani, upendo,
umoja na mshikamano kwa maendeleo ya nchi.
“Ninaomba kuchukua nafasi ya pekee
kuwaomba wananchi wote waliopo Dodoma kujitokeza kwa wingi uwanja wa Jamhuri
siku hiyo ya Jumatano tarehe 26 Aprili 2017 kuanzia saa 12:00 asubuhi ili
kusherehekea kwa pamoja maadhimisho hayo muhimu kwa nchi yetu,”alisema Jenista Mhagama.
Maadhimisho ya
Muungano yanafanyika kwa mara ya kwanza Dodoma ikiwa ni siku kadhaa tangu
Serikali ya Awamu ya Tano ianze kutumiza azma ya kuhamia katika makao makuu
hayo mapya
No comments