JAMHURI YAOMBA KUONDOA KESI YA KUJIFANYA AFISA USALAMA YA ALIYEKUWA MWENYEKITI UVCCM ARUSHA
Upande
wa Jamuhuri umeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi
ya jijini Arusha kuiondoa kesi ya kujifanya Afisa usalama wa Taifa na kujipatia chakula katika hotel moja ya kimataifa jijini Arusha
inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo Bw.
Akitoa
ombi hilo Wakili wa Serikali Bi. Grace Madikenya mbele ya Hakimu wa Mahakama ya
Hakimu mkazi Arusha, Mhe. Gwantwa Mwakuga, alisema upande wa Jamhuri hauna nia
ya kuendelea na kesi hiyo sababu shahidi mmoja muhimu yupo nje ya nchi kwa
miezi 18.
“Sasa tumeona tutamtesa mteja wetu. Hivyo kwa
nia njema kabisa tumeamua kuiondoa mahakamani kesi hii, maana miezi hii 18
ni mwaka mmoja na miezi sita,”alisema.
Ombi hilo lilipingwa vikali na Wakili wa
utetezi, Bi. Edna Haraka na kuiomba mahakama hiyo iendelee na kesi hiyo, kwa
madai kuwa upande wa mwendesha mashitaka unatumia Mahakama kama kichaka cha
kumnyima haki mteja wao na kumnyanyasa.
Alisema
upande huo hauna nia njema na mshitakiwa na kwamba kitendo cha kuiondoa kesi
hiyo mahakamani sio mara ya kwanza ni mara ya pili, ambapo ya kwanza waliomba
hivyo na mahakama ilipofuta walimkamata mteja wao na kumnyima dhamana.
“Sasa
leo tupo katika kusikiliza shahidi wa tatu na badala ya kuleta shahidi walileta
maelezo ya shahidi na leo wanakuja na stori ya kuiondoa ili waendelee
kumyanyasa mteja wetu. Hapana! Ofisi hiyo ya Mwanasheria Mkuu inatumika vibaya
kwa kivuli cha Mahakama,”alisema Edna
Wakili
huyo alisema serikali ya sasa inasisitiza mpango wa kuharakisha mashauri
kusikiliza wa BRN, sasa wakati inafanyika hivyo wengine wanachelewesha kwa
sababu zao.
Hakimu
Gwantwa Mwakuga baada ya kusikiliza pande zote mbili, alisema atatoa uamuzi
Aprili 28 mwaka huu, ya kama anakubali
shauri liondolewe au la.
Bw. Lengai anakabiliwa na shitaka la kujifanya
Afisa Usalama wa Taifa na kujipatia huduma ya chakula na malazi kwenye Hotel ya
kimataifa ya Highway ya jijini Arusha.
No comments