Sakata La Kuvamia Mkutano Wa Waandishi Wa Habari Cuf Yaomba Radhi
Siku chache zilizopita
baada ya kutokea fujo kwenye mkutano wa CUF uliokuwa umeandaliwa na upande wa
wafuasi wa Maalim Seif Sharif Hamad, upande ambao upo chini ya prof lipumba umejitokeza
na kukiri na kuomba radhi hadharani kuwa vijana waliofanya fujo katika mkutano
huo walikuwa ni walinzi wa chama hicho cha CUF.
Akizungumza Makao Makuu
ya Chama hicho yaliyopo Buguruni Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa Habari
wa CUF, Abdul Kambaya alisema vijana
waliofanya fujo kwenye mkutano huo walikuwa ni walinzi wa chama hicho ambao
walikuwa katika doria.
Amesema kuwa vijana
walikuwa katika doria la kawaida kwani tayali walikuwa wameshapata taarifa za
mkutano huo ambao haukutakiwa kufanyika mujibu wa katiba ya chama hicho.
“Mtu yeyote asipindishe
kitu, wale hawakuwa majambazi, ni vijana wetu wa CUF na walikuwa kwenye doria kwa
sababu tulikuwa na taarifa tayali juu ya
mikakati yao waliyoipanga na Chadema, hatuwezi kupangiwa mipango na Ukawa
wakati sisi ni Chama halali,”amesema Kambaya.
Aidha, Kambaya
ameongeza kuwa mchezo mchafu anaoucheza Meya wa Ubungo, Boniface Jacob na
Chadema kwa ujumla wa kutaka kuisambaratisha CUF hautafanikiwa.
Hata hivyo, katika
hatua nyingine, Kambaya amesema kuwa Chama Cha Wananchi (CUF), kinaomba radhi
kwa waandishi wa habari, Jukwaa la Wahariri pamoja na vyombo vyao kwa tukio
hilo lililosababisha taharuki kubwa.
msikilize hapa akiongea.....
No comments