WATUHUMIWA WA UGAIDI WATISHIA KUGOMA MAHAKAMANI

Mahakama ya Hakimu
Mkazi Arusha leo imesikiliza malalamiko ya watuhumiwa 61 wanao kabiliwa na kosa
la ugaidi, ambapo ni shauri lililofunguliwa mwaka 2014.
Wakizungumza leo
mahakamani hapo watuhumiwa hao wamesema kuwa leo ndiyo itakuwa mwisho wao
kufika kwenye viwanja vya mahakama hiyo mpaka upande wa jamuhuri utakapo
kamilisha upelelezi wao.
Wamesema wamekuwa
wakifika mahakamani kwa muda ambapo wengi wao familia zinateseka na
kusambaratika sababu ya kukaa mahabusu kwa miaka minne kwa makosa ya
kusingiziwa.
Aidha wamesema wamekuwa
wakipewa ahadi hewa na mkuu wa
upelelezi kuwa angeshughulikia shauri
hilo ndani ya miezi mitatu na kwamba suala la mahakama kushindwa kutekeleza
wajibu wake wa kikatiba linaleta ukakasi
kwa wananchi.
Hakimu Mfawidhi Nestory
Baro wa mahakama hiyo amewataka watuhumiwa kuwa na subira wakati
wakishughulikia shauri lao ambapo kesi itatajwa April 11 mwaka huu na amewataka
kufika mahakamani siku hiyo bila kukosa wakati akifanya utaratibu wa kumtafuta
mkuu wa upelelezi na kuzungumza naye
Post Comment
No comments