VIDEO: WAZIRI MKUU MAJALIWA ATUA BUZWAGI NAKUONDOKA NA MCHANGA WA MADINI

Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa ametinga kwenye mgodi wa dhahabu wa Buzwagi uliopo Kahama mkoani
Shinyanga na kuchukua sampuli za mchanga kwa lengo la kwenda kuyapima kwa
wataalamu wa madini ili kubaini kiasi cha dhahabu kilichomo.
Amesema wanataka kuona
mchanga unaosafirishwa na mwekezaji huyo una kiasi gani cha dhahabu, pia
Serikali inataka kufahamu kama kodi inayolipwa ni sahihi.
“Tumeamua kuchukua
sampuli za mchanga ambao mwekezaji anasema wanaupeleka nje ya nchi kwa ajili ya
kwenda kutenganisha madini ya dhahabu na shaba. Hata hivyo nimemuhoji kwa nini
mitambo hiyo isiletwe nchini ili kila kitu kifanyike hapahapa,” Amesema
Majaliwa
Waziri Mkuu amesema
sera ya uwekezaji inasema mtambo huo unatakiwa uwepo nchini ili kila hatua ya
uchenjuaji ifanyike hapa hapa, hivyo tunataka kujiridhisha na mwenendo wa
mwekezaji na mapato tunayoyapata kama yanastahili.
Aliongeza kwamba “Hili
lipo miongoni mwa masharti ya uwekezaji kwenye sekta ya madini nchini kwamba
mitambo hiyo ije kujengwa hapa nchini na itaongeza fursa ya ajira na kukuza
sekta nyingine ikiwemo ya kilimo,”.
Kuhusu uzalishaji
mgodini hapo
Kwa upande wake Meneja
Uendelezaji wa mgodi huo Bw. George Mkanza alisema mgodi huo ulionzishwa mwaka
2009 umeajiri watumishi 720 pamoja na vibarua 500.

Alisema kwa siku
wanachenjua makontena matatu hadi sita ambapo katika kila kontena moja wanapata
kilo tatu za madini ya dhahabu na tani nne za madini ya shaba.
Bw. Mkanza alisema
wanazalisha asilimia 50 ya madini ya dhahabu na asilimia 50 ya dhahabu iko
kwenye mchanga na inakuwa imechanganyika na madini ya shaba ambayo ndiyo
unaosafirishwa kwenda nje ya nchi kwa ajili ya kutenganishwa.
“Hapa Buzwagi tuna
makontena 179, makontena mengine 152 yako Dar es Salaam kwenye bandari kavu ya
Nazam na 21 yako bandarini. Kila siku tunapoendelea kuzalisha tunakuwa na
makontena manne hadi sita. Ndugu zetu wa Bulyanhulu nao wanamakontena 108 yako
mgodini na 104 yako Nazam Cargo Dar es Salaam,” alisema.
Post Comment
No comments