MOHAMMED RAZA AJITOSA VITA DHIDI YA DAWA ZA KULEVYA
Kada
wa Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya Kati,Mkoa wa
Kusini Unguja akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Jijini
Dar es Salaam, kuhusu kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano chini ya
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe Magufuli katika vita dhidi ya dawa za
kulevya nchini.
Kada
wa Chama cha Mapinduzi na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, wilaya ya Kati,Mkoa wa
Kusini Unguja akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya
Habari - MAELEZO leo Jijini Dar es Salaam, kuhusu kuunga mkono juhudi za
Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt. John Pombe
Magufuli katika vita dhidi ya dawa za kulevya nchini. Picha na: Frank Shija –
MAELEZO.
Na.
Lilian Lundo – MAELEZO
Kada
wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini, Mkoa wa Kusini
Unguja, Mhe. Mohammed Raza ameunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya
inayoendeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano.
Raza
ameyasema hayo leo, Mjini Dar es Salaam alipokuwa akiongea na vyombo vya habari
juu ya vita hiyo ya dawa za kulevya inayoendelea nchini.
“Naunga
mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John
Pombe Magufuli ni imani yangu vita hii dhidi ya dawa za kulevya tutaishinda,
kama tulivyomshinda nduli Idd Amini,” alifafanua Raza.
Aliendelea
kwa kusema kuwa, kila Mtanzania anatakiwa kuwa na uchungu na nchi yake kwa
kuunga mkono vita dhidi ya dawa za kulevya kwa kuwa biashara hiyo inadhoofisha
nguvu ya Taifa.
Aidha
amesema kuwa dawa za kulevya ni janga la Dunia nzima na uwezo wa kuliondosha
kwa Tanzania unahitaji ushirikiano wa Serikali zote mbili za Tanzania Bara na
Visiwani na wananchi wake.
Hata
hivyo, Raza ameiomba Serikali kununua vifaa vya kisasa vitakavyosaidia kutambua
dawa za kulevya ili kuzuia uingizaji wa dawa hizo hapa nchini, hasa kwa Zanzibar
ambayo imezungukwa na bahari hivyo kurahisisha uingizaji kutokana na kutokuwepo
kwa vifaa hivyo.
Katika
hatua nyingine Raza amempongeza Rais Dkt. Magufuli kwa kurejesha maadili kwa
watanzania na viongozi tofauti na ilivyokuwa hapo zamani.
Amesema
kuwa haikuwa rahisi kwa mtoto wa mkulima kupata ajira lakini kwa Serikali Awamu
hii watanzania wote wamekuwa na thamani bila kubaguliwa kutokana na kipato,
rangi, kabila au dini zao.
No comments