KUTOKA JIJINI MWANZA; VURUGU MGAMBO NA MACHINGA ZAIBUKA TENA
Vurugu
na mvutano mkali umeibuka jana kati ya mgambo wa jiji la Mwanza na wamachinga
wanaofanya biashara katika eneo la Makoroboi baada ya kutakiwa kuondoka mahali
hapo.
Eneo
hilo lipo katikati ya msikiti unaomilikiwa na watu wenye asili ya Asia wa
Swaminarayan na Shule ya watoto wadogo ya Tample.
Uamuzi
huo umekuja wakati tayari Rais John Magufuli alishaonya kutowavumilia viongozi
wa mikoa watakaowaondoa wamachinga kwenye maeneo yao, kabla hawajawatafutia
maeneo mbadala ya kufanyia biashara.
Katika
vurugu hiyo iliyotokea asubuhi jana inadaiwa kuwa mgambo mmoja alijeruhiwa
baada ya kushambuliwa na wamachinga hao wakipinga kuondolewa eneo hilo.
Hata
hivyo, walipotafutwa viongozi husika kuzungumzia tukio hilo hawakupatikana kwa
madai wapo kwenye vikao.
Hivi
karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiomoni Kibamba
aliwatangazia wamachinga wote ambao wapo katika maeneo yasiyo rasmi waondoke
kufikia Februari 9, mwaka huu na kwamba atakayekaidi ataondolewa kwa nguvu.
Wakizungumza
katika eneo la tukio, baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo, walisema hatua hiyo
ilijitokeza baada ya kutakiwa kuondoka katika eneo hilo.
“Tulipofika hapa asubuhi tulikuta, sehemu
tunayopanga bidhaa zetu kuna mgambo wa jiji wakisema hakuna mtu kuingia wala
kufungua biashara eneo hilo, mgambo walianza kutufukuza,” alisema Ally Erick.
Shuhuda
mwingine alisema kutokana na hasira waliyoipata watu hao walilazimika nao
kujihami kwani mgambo hao walishindwa kutumia busara baada ya kutaka kuwaondoa
kwa kuwapiga virungu.
Alisema
baada ya kuzidiwa walilazimika kuomba nguvu mpya kutoka kwa askari wa kutuliza
ghasia.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema yupo kwenye kikao na Kaimu
Mkurugenzi wa jiji la Mwanza, Hosiana Kosiga alisema naye yupo kwenye kikao.
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana, Merry Tesha alisema hayupo eneo lake la kazi badala
yake atafutwe Mkuu wa Wilaya ya Ilemela anayekaimu nafasi hiyo, Dk Leonal
Masale,hata hivyo alipopigiwa simu iliita bila kupata majibu.
No comments