TAARIFA KUTOKA KATIKA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM JIJINI DAR ES SALAAM LEO
TAARIFA KWA
VYOMBO VYA HABARI
Halmashauri
Kuu ya Taifa ya CCM imekutana leo tarehe 13/12/2016 jijini Dar es salaam kwa
kikao cha siku moja cha kawaida. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Taifa
wa CCM Dkt. John Pombe Magufuli.
Pamoja na
mambo mengine, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM imepokea taarifa ya Tathimini ya
Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, baada ya kuitafakari taarifa hiyo, Halmashauri Kuu
imeamua yafuatayo;-
1. Kupunguza
idadi ya wajumbe wa vikao na idadi ya vikao vya Chama katika ngazi mbalimbali
ili kuongeza ufanisi wa utendaji wa Chama na kuongeza muda wa viongozi wa Chama
kufanya kazi za Chama kwa Umma badala ya kutumia muda mwingi vikaoni.
Ili
kuwa na vikao vya Chama vyenye tija
imeamuliwa kama ifuatavyo:-
a). Halmashauri
Kuu ya Taifa kwa sasa ina jumla ya wajumbe 388 idadi ambayo ni kubwa sana,
hivyo imeamuliwa idadi hii ipunguzwe na kuwa wajumbe 158 kama ifuatavyo:-
Wenyeviti wa Mikoa
Mikoa ya
Bara 26x1 = 26
Mikoa ya
Zanzibar 6x1 = 6
Wajumbe wa
NEC wa Mikoa
Mikoa ya Bara 26x1 = 26
Mikoa ya Zanzibar 6x4 = 24
Wajumbe wa
NEC wa Taifa
Kutoka
Bara = 15
Kutoka
Zanzibar
= 15
Nafasi za
Mwenyekiti = 7
Wajumbe wa
NEC wa Jumuiya
UVCCM
= 5
UWT
= 5
WAZAZI
= 5
Wajumbe wa
NEC kutoka Bungeni = 5
Katibu wa
Kamati ya Wabunge wa CCM = 1
Wajumbe wa NEC kutoka BLW = 3
Katibu wa
Kamati ya Wawakilishi
= 1
Wajumbe wa
NEC – wanaotokana na Nyadhifa zao
- Mwenyekiti
wa CCM = 1
- Makamu
Mwenyekiti (B) = 1
-Makamu
Mwenyekiti (Z) = 1
- Makamu wa
Rais = 1
- Waziri Mkuu = 1
- Makamu wa
Pili wa Rais (Z) = 1
- Spika wa
Bunge = 1
- Spika wa
BLW
= 1
- Mwenyekiti
wa UWT = 1
- Mwenyekiti
wa WAZAZI = 1
-Mwenyekiti
wa UVCCM = 1
- Katibu
Mkuu – WAZAZI = 1
- Katibu
Mkuu – UWT =
1
- Katibu
Mkuu – UVCCM = 1
Jumla: 158
#. Vikao vya
kawaida vya Halmashauri Kuu ya Taifa vifanyike kila baada ya miezi sita badala
ya miezi minne kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum
inapohitajika.
b). Kwa
upande wa sasa imeamuliwa wajumbe wa Kamati Kuu wawe 24 badala ya 34 kama
ifuatavyo:-
Mwenyekiti
wa CCM.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Bara)
Makamu
Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar)
Makamu
wa Rais
Katibu Mkuu
wa CCM
Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Bara)
Naibu Katibu
Mkuu wa CCM (Zanzibar)
Waziri Mkuu
Makamu wa
Pili wa Rais (Z)
Spika wa
Bunge la Tanzania
Spika wa BWL
Mwenyekiti wa WAZAZI
Mwenyekiti wa UWT
Mwenyekiti wa UVCCM
Katibu
wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Organaizesheni
Katibu
wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Itikadi na Uenezi
Katibu
wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Uchumi na Fedha
Katibu
wa wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Mambo ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa
Wajumbe watatu (3)
wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu
kutoka Tanzania
Wajumbe
watatu (3) wa kuchaguliwa na Halmashauri Kuu kutoka Zanzibar.
#. Vikao vya
kawaida vya Kamati Kuu vipunguzwe ili vifanyike kila baada ya miezi minne badala ya miezi miwili
isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
c). Kwa
ngazi ya mkoa, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Mikoa wapunguzwe kwa kuondoa
wajumbe watatu ambao ni:-
Katibu wa
Uchumi na Fedha wa Mkoa - 1
Wajumbe wa
kuchaguliwa na H/Mkoa -
2
#.
Vikao vya kawaida vya Kamati ya Siasa ya
Mkoa vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi kama ilivyo sasa isipokuwa vinaweza
kufanyika vikao maalum inapohitajika.
d). Kwa
upande wa Wilaya Wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya wapunguzwe kwa
kuwoandoa:-
Katibu wa Uchumi na Fedha wa Wilaya -
1
Katibu wa Kamati ya Madiwani - 1
Wajumbe wa kuchaguliwa na H/Kuu ya (W)- 2
Jumla: 4
#.Vikao vya kawaida
vya Kamati ya Siasa ya Wilaya
vifanyike kila baada ya miezi mitatu badala ya kila mwezi isipokuwa vinaweza kufanyika vikao
maalum inapohitajika.
#. Muundo wa
Wilaya za Chama uendane na muundo wa sasa wa Serikali.
Kata,Tawi na
ShinaIdadi ya kuanzisha Shina iwe wanachama 50
hadi 300.
Idadi ya
kuanzisha Tawi iwe wanachama kuanzia 301 hadi 1,000.
Hata hivyo
idadi hii izingatie eneo la kijiografia na wingi wa wanachama katika eneo hilo.
Vikao vya
kawaida vya Kamati za Siasa za
ngazi hizi viwe vinafanyika mara moja kila baada ya miezi mitatu,
isipokuwa vinaweza kufanyika vikao maalum inapohitajika.
#. Nafasi za
Uongozi
Mwanachama
anatakiwa kuwa na nafasi moja tu ya
uongozi wa kazi za muda wote kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni za uchaguzi wa
Chama Toleo la 2012 kifungu cha 22 na 23 ambazo zimetajwa kuwa ni:-
Mwenyekiti
wa Tawi,Kijiji au Mitaa.
Mwenyekiti
wa Kata/Wadi.
Mwenyekiti
wa Jimbo, Wilaya na Mkoa.
Makatibu wa
Halmashauri Kuu wa ngazi zote zinazohusika.
Mbunge,
Mwakilishi na Diwani.
#. Viongozi
wa kuchaguliwa waepuke kuwa watendaji badala yake waongoze na kusimamia
shughuli za Chama kwa kuzingatia Katiba na Kanuni.
#.Vyeo
ambavyo haviko kwenye Katiba
Vyeo ambavyo havijatamkwa kwenye Katiba ya CCM
haviruhusiwi katika Chama au Jumuiya zake mfano Umoja wa makundi mbalimbali
kama Wenyeviti wa ngazi mbalimbali (mfano: Mwenyekiti wa Wenyeviti wa CCM n.k),
Makamanda (UVCCM), Washauri (UWT) na Walezi (WAZAZI) katika ngazi zote.
#. Uhakiki
wa Wanachama wa CCMHalmashauri Kuu imeona ipo haja ya kufanya uhakiki wa
wanachama wa CCM na Jumuiya zake ili
kujua idadi sahihi ya wanachama wetu kwa wakati huu. Uhakiki huu uendane na kutoa kadi mpya za
uanachama za kielektroniki ili kuwa na udhibiti wa usahihi wa wanachama na
kuondoa wanachama HEWA. Aidha, Kadi za UWT, WAZAZI na UVCCM zifutwe ili tubaki
na kadi za CCM tu.
#. Jumuiya
za Chama Cha Mapinduzi
Jumuiya za
CCM zimetakiwa kufanya kazi zake kwa
kuzingatia matakwa ya Katiba ya CCM na Kanuni za Jumuiya husika, kanuni za
Jumuiya ziendane na matakwa ya Katiba ya
CCM.
#.Uaendeshaji wa shughuli zote za Jumuiya za Chama na mali
zake uwe chini ya usimamizi wa Chama Cha Mapinduzi. (Baraza la Wadhamini la
Chama Cha Mapinduzi).
Makatibu
Wakuu wa Jumuiya watakuwa wanateuliwa na Kamati Kuu na
Manaibu Katibu Wakuu watateuliwa na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya
Taifa.
#. Wakati
tukiendelea kubaki na Bendera yenye
rangi ya kijani na njano na alama ya jembe na nyundo, Halmashauri Kuu
imeona ipo haja ya kuzifanya rangi hizo kuwa na muenekano wa kuvutia zaidi.
#.
Utumishi katika Chama na Jumuiya zake. Katibu Mkuu wa CCM na
Sekretarieti ipewe majukumu ya kusimamia ajira za Watumishi wa Chama na Jumuiya
zake.
Nafasi za
Makatibu Wasaidizi wa Mikoa na Wilaya zitaondolewa na badala yake kazi zao
zitatekelezwa na Makatibu wa Jumuiya za
Chama wa Mikoa na Wilaya kwa utaratibu utakaopangwa. Utaratibu huu utakipunguzia Chama Cha
Mapinduzi gharama na kujenga umoja wa utendaji kazi wa Chama na Jumuiya zake
katika Mikoa na Wilaya.
#. Tathimini
ya hali ya Kisiasa na Uchaguzi wa Zanzibar .Halmashauri Kuu ya Taifa imeagiza
kuundwa kwa Kamati maalum ya kufanya tathimini ya kina kuhusu hali ya kisiasa
Zanzibar kwa ujumla na masuala yanayohusu uchaguzi wa Zanzibar 2015.
# Mwenyekiti
wa Kamati ya udhibiti na nidhamu ametakiwa akamilishe kazi ya taarifa ya
udhibiti kwa wanachama waliokiuka mienendo ya kiuanachama kabla ya kuanza
uchaguzi Mkuu wa Chama mwezi Februari 2017, Mikoa na Wilaya ambazo hazijaleta
taarifa zao za kiudhibiti ziwe zimefikisha taarifa zao kwa Mwenyekiti wa Kamati
ya Udhibiti na Nidhamu kabla ya tarehe 30/01/2017.
#. Uhakiki
wa Mali za Chama uendelee kufanyika kwa kina na uchambuzi zaidi ukikamilika
Taarifa yake iwasilishwe kwa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa mapema
iwezekanavyo.
#. Maamuzi
na mapendekezo haya yatapelekea kufanyika kwa mabadiliko ya Katiba ya Chama na
Kanuni za Jumuiya za Chama.
#. Kwa mambo
yale ambayo yatahitaji mabadiliko ya Katiba, Mkutano Mkuu utaandaliwa mapema
mwakani na kutafakari na kupitisha mabadiliko hayo ya Katiba.
Mwenyekiti
wa CCM Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameteua wafuatao kujaza nafasi
mbalimbali ndani ya sekretarieti ambazo zimekuwa wazi kutokana na waliokuwa
wakizishikilia kupewa majukumu mengine ya kiserikali.
#.Ndg.
Rodrick Mpogolo anakuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuchukua nafasi
iliyoachwa wazi na Ndg. Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi.
#. Col.
Ngemela Eslom Lubinga- Kuwa Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa kujaza
nafasi iliyoachwa wazi na Dr. Asha-Rose Migiro aliyeteuliwa kuwa Balozi
#. Humphrey
Polepole kuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi kujaza nafasi iliyoachwa wazi na
Ndg. Nape Nnauye aliyeteuliwa kuwa Waziri.
#. Wajumbe
wengine watabaki kama walivyo sasa.
Imetolewa na:-
NAPE NNAUYE
IDARA YA ITIKADI NA UENEZI
13/12/2016
No comments