Breaking News

MAUZO YA HISA KATIKA SOKO LA HISA DAR ES SALAAM (DSE) YAMEPANDA YA MARA 6 ZAIDI WIKI HII.

Afisa mwandamizi wa soko la hisa Dar es Salaam, Bi Marry Kinabo

Na Frank wandiba
Mauzo katika soko la Hisa la Dar es salaam (DSE)  yamepanda mara 6 zaidi kutoka TZS 198 Millioni mpaka kufikia Tshs  1.22 billioni wiki hii iliyoishia tarehe 9 Disemba mwaka huu.

Akiwasilisha taarifa za mwenendo wa soko kwa wiki iliyoishia Ijumaa tarehe 8 mwezi huu mapema leo jijini dar es salaam, Afisa mwandamizi wa soko la hisa Dar es Salaam, Bi Marry Kinabo alisema Idadi ya Hisa  pia imeongezeka kwa asilimia 44%, kutoka Hisa 262,598 wiki iliyopita mpaka 378,149 wiki hii.
Alisema kwa upande wa ukubwa wa mtaji wa makampuni kwa ujumla umeshuka kwa asilimia 0.5%, kwa upade wa makampuni ya ndani umeendelea kubaki kwenye kiwango kile kile cha Trilioni 8.

Aidha Bi, Kinabo amezitaja kampuni tatu zilizoongoza kwa idadi ya Hisa zilizouzwa na kununuliwa kwa wiki iliyopita kuwa ni  Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) kwa asilimia 47%, ikifatiwa na Benki ya DCB kwa asilimia 19%  na TBL kwa asilimia 18%.
Pia aliongeza kuwa viashiria katika Sekta ya viwanda imeshuka kwa pointi 104.63, kwa upande wa Sekta ya Huduma za Kibenki na Kifedha imeshuka pia kwa pointi 3.66, wakati kwa upande Sekta ya Huduma za Kibiashara wiki hii imeendelea kubaki kwenye wastani ule ule wa TZS 3,157 sawa na wiki iliyopita

No comments