MADEREVA BODABODA VINARA WA KUBAKA, KULAWITI NA KUWAPA MIMBA WANAFUNZI
MADEREVA
wa bodaboda wametajwa kuongoza kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani
Pwani yanayohusisha ubakaji, ulawiti na kuwapa mimba wanafunzi.
Imeelezwa
kuwa, kati ya watuhumiwa 10 wa makosa hayo ya ukatili, watatu ni madereva wa
bodaboda.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Pwani, Bonaventura Mushongi, alisema hayo alipokuwa
akizungumza na madereva wa bodaboda na wananchi na kusema kuwa hilo ni janga
ambalo linapaswa kupigiwa kelele na jamii yote.
Alisema
matukio ya ukatili wa kijinsia mkoani Pwani yameongezeka kutoka 257 kwa kipindi
cha Januari hadi Septemba mwaka jana na kufikia 310 kipindi kama hicho mwaka
huu, ikiwa ni ongezeko la makosa 53.
Aidha
imebainika kuwa madereva wa bodaboda wanaongoza kwa kufanya matukio hayo ya
ukatili wa kijinsia ikiwa ni pamoja na ubakaji, ulawiti, kuwapa mimba
wanafunzi.
Kamanda
Mushongi alisema utafiti uliofanywa na dawati la jinsia na watoto mkoani hapo,
limebaini kwamba baadhi ya madereva bodaboda hujihusisha na vitendo hivyo jambo
ambalo linapaswa kupigwa vita.
“Madereva
hao wasaidiane kuwafichua wale ambao wamekuwa wakiitia doa kazi hiyo na
kuwachafua mbele ya uso wa jamii na kuanzisha timu za ulinzi na usalama ili
kupeana elimu na kutoa taarifa juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia,”
alisema.
Alisema
kupitia umoja wao wapinge matendo yote ya ukatili na udhalilishaji na kuwalinda
watoto ili kupambana dhidi ya vitendo vya ukatili kwa lengo la kupunguza na
kutokomeza vitendo hivyo.
Hata
hivyo, Mushongi aliwaomba wazazi kuhakikisha wanasimamia malezi ya watoto kwa
karibu, badala ya kuwaachia kina mama pekee ambao baadhi yao huwaachia
wasichana wa kazi jukumu hilo.
Alibainisha
suala hilo la wazazi kuwa mbali husababisha baadhi ya watoto kujitumbukiza
katika vitendo vya ngono wakiwa katika umri mdogo na kusababisha kupata
ujauzito, ama kuambukizwa magonjwa ikiwemo virusi vya Ukimwi.
Source habari
leo
|
No comments