NAPE NNAUYE NAWAOMBA RADHI VIONGOZI NA WAFUASI WA VYAMA VYA UPINZANI TANZANIA
Alikuwa
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Nape Nnauye amewaomba
radhi viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani nchini kwa lolote ambalo
aliwakwaza wakati akitekeleza majukumu yake katika nafasi hiyo.
Nape
amewaangukia wapinzani pamoja na makundi mengine ya watanzania ikiwemo viongozi
wenzake ndani ya chama leo wakati akikabidhi rasmi ofisi kwa kiongozi mpya
anayechukua nafasi hiyo, ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Dar es Salaam,
Humphrey Polepole katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho, Lumumba
Jijini Dar es Salaam.
"Nawaomba
msamaha viongozi wenzangu, wanachama, waandishi na hata wapinzani pale ambapo
nimewaumiza katika kufanya kazi yangu, samahani sana. Nategemea ushirikiano
niliopatiwa mimi na wanahabari utaendelea kwa ndugu yangu Humphrey Polepole, ni
mtu mwenye weledi mpana" amesema Nape
Nape
pia amekiri kuwa chama hicho kimemsaidia zaidi kwenye maisha yake kuliko yeye
alivyokisaidia wakati akiitumikia nafasi hiyo.
"Nakiri
mbele yenu kuwa chama kimenisaidia zaidi kuliko mimi nilivyokisaidia Chama,
nashukuru Mungu kuwa nimemaliza kazi hii salama, nilipata wosia wa Mzee Kinana
kuwa nishukuru nikimaliza salama"
|
No comments