WAHAMIAJI HARAMU 13 WANASWA WAKIFANYA BIASHARA YA UKAHABA DAR
Idara ya Uhamiaji Mkoa
wa Dar es Salaam imewakamata wasichana 13 kutoka nchi za Nebal na India wenye
umri kati ya miaka 18 na 26 ambao wameletwa nchini kinyume cha sheria na
kuendesha biashara ya ukahaba katika jijini humo.
Akiongea na waandishi wa
habari leo mara baada ya kufanya oparesheni ya kufunga madanguro yote na
kuwasaka raia wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha Sheria, Kamishna wa
Uhamiaji Kanda ya Dar es Salaam John Msumule amesema mbali na raia hao wa
kigeni pia wamewamakata raia wa Kitanzania mbao wanashirikiana na wahamiaji
hao.
Amemtaja Bwana Mohamed
Shabani Magamba ambaye anatengeneza vibali vya kugushi ambapo pia amekutwa na
pastpoti 4 za raia wa nchi za Nigeria, Botswana, Somalia na Uingereza.
Bwana Msumule ameitaja
Wilaya ya Kinondoni kuwa inaongoza kwa kuwa na Madanguro ikifuatiwa na Temeke
ambapo kwa sasa wanajipanga kuyaondoa kwa muda wa siku 10 madanguro hayo pamoja
na kuendesha oparesheni kubwa katika Mitaa ya Msimbazi, Lumumba na Uhuru katika
soko la Kariakoo na maeneo ya Mtoni Mtongani na Sabasaba ambako wamekwisha
yafanyia uchunguzi wa kina.
|
No comments