WANANCHI WAHAMASHWA KUSHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI KUCHANGIA WAHANGA WA TETEMEKO LA KAGERA
Mkuu wa
kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika
Mashariki Bi. Mindi Kasiga
Na.
Immaculate Makilika- MAELEZO
Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana
na Ofisi ya Waziri Mkuu imeandaa matembezi ya hisani ili kusaidia
wahanga waliokumbwa na maafa ya tetemeko la
ardhi lilitotokea Septemba 10 mwaka huu, huko
mkoani Kagera.
Akizungumza na
waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bi. Mindi Kasiga
amesema kuwa, matembezi hayo ya hisani ya kilomita tano yataongozwa na Rais Mstaafu
wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Aliongeza kuwa Matembezi
hayo yatafanyika siku ya Jumamosi Septemba17 mwaka huu, ambapo yataanzia Bwalo
la Polisi Osterbay (Polisi Officer’s Mess) kuanzia saa 12 asubuhi.
Aidha amesema kuwa,
matembezi hayo yana lengo la kuhamasisha wafanyabiashara, taasisi za fedha,
kampuni mbalimbali pamoja na jamii ya watanzania, wanadiplomasia
waliopo nchini kuchangia kwa kutoa misaada mbalimbali ili kusaidia wahanga
maafa ya tetemeko la ardhi la mkoani Kagera.
“Tunafanya kampeni hii ya
tembea kwa ajili ya Kagera, kwa lengo la kuwahamasisha watanzania,
wafanyabashara na jumuiya ya wanadiplomasia waliopo nchini ili kila mtu aweze
kushiriki kwa kuchangia kiasi chochote cha fedha kitakachosaidia wenzetu
waliokumbwa na maafa ya tetemeko la ardhi lililotokea Kagera” alisema Kasiga
Hivyo basi, Wizara hiyo
imeeandaa daftari maalumu la michango kwa jumuiya ya mabalozi katika
nchi zote zenye Ofisi za Ubalozi wa Tanzania, ili kuunga mkono zoezi la
kuwasaidia wahanga wa maafa ya tetemeko la ardhi lilitokea mjini Bukoba.
Pia Serikali imefungua
akaunti rasmi kwa jina la Kamati Maafa Kagera katika benki ya CRDB
ya mkoani Kagera yenye namba 0152225617300 ambayo itakayotumika
kupokea michango kutoka kwa watu mbalimbali.
No comments