NAIBU MEYA ILALA, MHE OMARY NGUMILAMOTO KAMPUNI YA UJENZI YA DEL-MONTE KUONDOLEWA KATIKA LIST TENDA ZA UJENZI KATIKA MANISPAA HIYO.
Naibu meya wa
Manispaa ya Ilala, Mhe Omary Ngumilamoto akisikiliza maelezo toka kwa kaimu Mhandisi
wa manispaa ya ilala mhandisi Nyamagulula Masatu katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ya
ujenzi iliyo chini ya manspaa hiyo
Naibu
meya wa Manispaa ya Ilala, Mhe Omary Ngumilamoto akisikiliza maelezo kutoka kwa mkandarasi wa kampuni ya
ujenzi ya Del Monte Bw Leornad Maguyani katika ziara
ya kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya manspaa hiyo.
Mkandarasi
wa kampuni ya ujenzi ya Del monte Bw Leornad
Maguyani akitoa maelezo juu ya mradi ujenzi wa barabara kutoka Mombasa hadi Mosha Baa kwa
kiwango cha Lami yenye urefu wa kilomotea 1.65 ambayo itagarimu Bilioni Sh 2.4 katika ziara ya wajumbe wa kamati ya fedha ya manispaa ya ilala kukagua miradi inayoendeshwa na manispaa hiyo
Wajumbe wa kamati ya fedha ya manispaa ya ilala
wakitembea kujionea ujenzi wa mradi wa barabra kutoka Mombasa hadi Mosha Baa
katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali iliyo chini ya manspaa hiyo.
Na Frank Wandiba
Naibu meya wa
Manispaa ya Ilala, Mhe Omary Ngumilamoto amesema wataiondoa Kampuni ya ujenzi wa Barabara Del-Monte katika tenda za ujenzi katika manispaa hiyo
baada ya kujiridhisha kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi chini ya kiwango pamoja
na kushindwa kumaliza kazi kwa wakati.
Kauli ya Mhe Ngumilamoto
inakuja ikiwa ni tayali mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe Paul Makonda ambaye aliagiza viongozi wote wa manispaa za
mkoa wa Dar es salaam kutopia tenda kampuni ya Del-Monte kutokana na
kujenga barabara nyingi chini ya kiwango.
Alisema Kampuni hiyo
ambayo imepewa tenda ya kujenga barabara kutoka Mombasa hadi Mosha Baa kwa
kiwango cha Lami yenye urefu wa kilomotea 1.65 ambayo itagarimu Bilioni Sh
2.4 ujenzi huo umekuwa ukisuasua ambapo
mpaka sasa kampuni hiyo tayali imeshalipwa milioni 301.
“Hii Kampuni ya
Del-monte tulishakamtaa kutokana na miradi mingi tunayompa kushindwa kumaliza
miradi kwa wakati licha ya kupewa fedha
lakini bado utendaji wake umekuwa usiolidhisha” alisema Ngumilamoto.
Ngumilamoto alisema
Halmashauri hiyo tayali ilishaingia Mkataba na kampuni hiyo hivyo hawezi
kumkatisha mkataba huo ila Mkataba wake utakoisha hawataendelea nayo sambamba
na kuiondoa kampuni hiyo katika listi ya kampuni zinazopewa tenda na Halmashauri
hiyo.
Aidha Mhe Ngumilamoto
amemtaka Kaimu Mhandisi wa Manispaa hiyo, Bw Nyamagulula Masatu kuhakikisha
anasimamia mradi huo unakamilika kwa wakati pamoja kuhusimamia ipasavyo
kutokana na miradi mingi ya Barabara kujengwa chini ya kiwango hivyo kuharibika
mda si mrefu tangu kukamilika kwa ujenzi wake.
Kwa Upande wake kaimu
mhandisi wa Manispaa ya Ilala Mhandisi
Masatu alimhakikishia Mhe, Ngumilamoto
kuwa ataisimamia mradi huo na
kuhakikisha itaisha kwa wakati.
No comments