MZEE MWINYI ASHIRIKI MATEMBEZI YA WALK FOR KAGERA ACHANGISHA SHILINGI BILIONI 1.5
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akizungumz wakati wa kufungua rasmi
Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera
“Walk For Kagera” leo Jijjini Dar es Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano
yalianzia katika viwanja vya Bwalo la Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla
ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi
Agustine Mahiga akizungumza na washiriki wa Matembezi ya Hisani kwa ajili ya
kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es
Salaam. Matembezi hayo ya kilomita tano yalianzia katika viwanja vya Bwalo la
Maofisa wa Polisi Osterbay ambapo jumla ya shilingi 1,502,680,000/= zilichangwa
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya
kuanza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani
Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine
Mahiga, Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Kagera, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Alhaj Ally Hassan Mwinyi akishiriki mazoezi ya viungo kabla ya
kuanza Matembezi ya Hisani kwa ajili ya kuchangia wahanga wa Tetemeko Mkoani
Kagera “Walk For Kagera” leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kutoka kulia ni
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Agustine
Mahiga, Mwenyekiti wa Wabunge kutoka Kagera, Profesa Anna Tibaijuka na Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi.
Naibu Waziri wa Nchi, OWM –Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi akizungumza katika hafla ya kuchangia
wahanga wa Tetemeko lililotokea mkoani Kagera iliyoandaliwa na Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya
Waziri Mkuu na Ikulu leo Jijini Dar es Salaam. Hafla hiyo iliyotanguliwa na
Matembezi ya Hisania ambapo kiasi cha shilingi 1,502,680,000/= kilipatikana.
![]() |
Akizungumza mara baada ya matembezi hayo Rais Mstaafu wa Awamu
ya Pili Mhe Ally Hassan Mwinyi aliwashukuru wadau mbalimbali
waliojitokeza na kushiriki matembezi hayo ya hisani.
“Nawapongeza sana wadau wote mlioshiriki katika matembezi haya,
mmeonyesha mshikamano mkubwa kwa umoja wenu mmeweza kuchangisha jumla ya
shilingi 1,502,680,000 hii inatia faraja sana muendelee na moyo huo” Alisema
Mzee Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi
amewahakikishia wananchi wa Mkoa wa Kagera kuwa Serikali inafanya kila
liwezekanalo kuhakikisha wahanga wa tetemeko hilo wanapatiwa huduma stahiki na
kwa wakati.
Balozi Kijazi aliongeza kuwa kutokana na kuguswa na tatizo hilo
Serikali pamoja na Taasisi zake imetoa msaada wake ambao unakadiriwa kuwa zaidi
ya shilingi bilioni moja ikiwa ni kuthamini utu wa wahanga.
“Najua kuna athari kubwa imetokea kutokana na tetemeko hili,
sisi kama Serikali tunafanya kila jitihada kuhakikisha wahanga wote wanapata
misaada na kurejesha huduma zote katika hali yake” Alisema Balozi Kijazi.
Awali akisoma maelezo ya tathmini ya athari za tetemeko hilo
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana,
Ajira na Walemavu Mhe. Abdallah Posi amesema kuwa hadi kufikia tarehe 16 idadi
ya vifo ni 17, nyumba zilizoanguka zimefikia 840 huku zilizoharibika zikiwa ni
1264 na majengo 44 mali ya Taasisi za umma yameharibika.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mabalozi nchi, Balozi wa Zimbabwe
ametoa pole kwa wahanga wa tukio hilo na kuahidi kuendelea kushirikiana na
Tanzania pale panapo hitaji msaada wao.
Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za
kusaidia wahanga wa tetemeko la Ardhi yaliandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki ,Ofisi ya Waziri Mkuu na Ikulu.
|
No comments