Breaking News

MHE. ANASTAZIA WAMBURA AZINDUA MAONESHO YA TAMTHILIA NA FILAMU ZA BEIJING LEO JIJINI DAR ES SALAAM.

mch1
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwasili katika Ukumbi wa Hayatt Regency Hotel kuzindua maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 Jijini Dar es Salaam.
mch2
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt Ayob Riyoba akizungumza na Mshauri wa masuala ya Utamaduni kutoka Jamhuri ya watu wa China Bw.Gao Wei wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 katika Ukumbi wa Hayatt Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
mch3
Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. Gou Haodong akizungumza na wadau wa Filamu na Thamthilia kutoka Tanzania na China wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 Jijini Dar es Salaam.
mch4
Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt Ayob Riyoba akizungumza na wadau wa Filamu na Thamthilia kutoka Tanzania na China wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 katika Ukumbi wa Hayatt Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
mch5
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akizungumza na wadau wa Thamthilia na Filamu kutoka Tanzania na China wakati wa uzinduzi wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 katika Ukumbi wa Hayatt Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
mch7
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Annastazia Wambura akimpongeza mshindi wa kwanza wa shindano la kuweka sauti katika tamthilia za kichina Bibi. Hilda Malecela mara baada ya uzinduzi wa  wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 katika Ukumbi wa Hayatt Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
mch9
Kikundi cha Utamaduni kutoka Tanzania kikitoa burudani kwa wageni waalikwa katika uzinduzi maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 katika Ukumbi wa Hayatt Regency Hotel Jijini Dar es Salaam. 
mch10
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa shindano la kuweka sauti katika Tamthilia za kichina mara baada ya uzinduzi  wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 Jijini Dar es Salaam.
mch11
Washindi wa shindano la kuweka sauti katika tamthilia za kichina wakishangilia ushindi wao mara baada ya kukabidhiwa vikombe na zawadi mara baada ya  uzinduzi  wa maonesho ya Tamthilia na Filamu za Beijing barani Afrika  Septemba 27,2016 Jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM)
……………………………………………………………..
Na: Genofeva Matemu – WHUSM
Filamu na tamthilia kutoka China zinazoingia nchini zimetakiwa kufuata na kuzingatia sheria za nchi ili ziweze kuendeleza utamaduni na uhusiano mzuri wa muda mrefu uliopo baina ya Tanzania na China.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia James Wambura wakati wa sherehe za uzinduzi wa maonesho ya Filamu na Tamthilia za China Barani Afrika leo katika Ukumbi wa Hyatt Regency Hotel Jijini Dar es Salaam.
“Watanzania wanafurahi sana na kupenda tamthilia na filamu kutoka China haswa pale wanaposikia mtanzania mwenzao ameigiza au amehusika katika kutafsiri filamu hizo” alisema Mhe. Anastazia.
Akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi Mhe. Anastazia amewashukuru Startimes kwa kuandaa mashindano ambayo wameyafanya hivi karibuni ya uigizaji wa sauti kuibua vipaji na kutoa fursa kwa watanzania kumi kwenda kuajiriwa nchini China katika makao makuu ya startimes Beijing.
Aidha Mhe. Anastazia amesema kuwa watanzania wamepata fursa ya kuangalia tamthilia na filamu za China kupitia king’amuzi cha startimes, chombo ambacho kimeweza kuenea kwa asilimia 80 kwa nchi za kusini mwa jangwa la sahara zilizotafsiriwa kwa lugha ya Kiswahili.
Mhe. Anastazia amesema kuwa tangu mwaka 2010 serikali kupitia mamlaka ya mawasiliano ilipoanzisha mfumo wa kidigitali makampuni mengi yamekua yakitumia mfumo huo kutoa huduma za kihabari nchini ambapo Startimes ni moja ya kampuni hizo ambayo imeweza kutoa masafa ya kidigitali katika kampuni binafsi na makampuni ya umma wakiwa na dira ya kutaka kuzifikia kaya ngingi iwezekanavyo ikiwezekana kaya zote nchini.
Naye Kaimu Balozi wa China nchini Tanzania Bw. GOU Haodong amesema kuwa filamu na tamthilia hutoa ajira kwa jamii kwani ni shughuli ambayo hutumia sanaa kufikisha ujumbe hivyo ni vyema waigizaji kutoka China pamoja na Tanzania kuheshimu kazi hiyo na kuwa kioo katika jamii wanayoishi.
Mwaka huu ni mwaka wa tatu tangu kuanzishwa kwa maonyesho ya filamu na tamthilia za kichina Barani Afrika. Maonyesho haya yanatambulisha kwa watazamaji wa Afrika tamthilia na filamu nyingi za kichina ambazo zimetafsiriwa kwa lugha za kiafrika na kusababisha kupendwa sana kwa tamthilia hizo barani Afrika.

No comments