MME NA MKE MBARONI KWA TUHUMA ZA UJAMBAZI JIJINI DAR
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya oparesheni ambazo zimefanyika maeneo mbalimbali na mafanikio yake leo jijini Dar es Salaam. ambapo Jeshi hilo lilifanikiwa kumtia mbaroni mtu mmoja kwa tuhuhuma za ujambazi wa kutumia silaha za moto.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionesha kwa wanahabari silaha zilizokamatwa kwa mtuhumiwa huyo.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Verosa likiwa limesheheni magunia saba za bangi leo iliyokamatwa hivi karibuni jiji Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha gari aina ya Noah ikiwa wan a magunia ya bangi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha namba za gari za bandia ambazo zimekuwa zikitumiwa na waharifu leo jijini Dar es Salaam. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, linawashikilia watu wawili ambao ni Mme
na Mke kwa tuhuma za matukio mbalimbali ya ujambazi wa kutumia silaha za moto
katika maeneo tofauti tofauti jijini Dar es salaam.
Watuhumiwa
hao ambao wametambulika kwa majina ya Bakari Abdallah (40) na Sihaba Omary (28)
wakazi wa Vijibweni, Kigamboni walitiwa mbaroni mnamo tarehe 23 Septemba mwaka
huu na Kikosi Maalum cha Jeshi hilo cha kupambana na ujambazi wa kutumia
silaha.
Akizungumza
mbele ya wanahabari, Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, Kamishna
Simon Sirro, alisema kuwa mnamo tarehe 26 Septemba mwaka huu Askari walifika
nyumbani kwa watuhumiwa hao na kukuta bastola aina ya "BROWNING"
yenye usajili namba CAR A081900 ikiwa na magazine mbili na risasi tano pamoja
na simu aina ya Nokia Lumia ambayo inadaiwa kuwa iliporwa katika matukio ya
unyang'anyi.
Watuhumiwa
wote wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano zaidi.
No comments