JAJI WARIOBA: VIJANA ENZINI NA KUENDELEZA AMANI NCHINI.
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wa kwanza
kulia akifungua pazia kushiria kuzindua rasmi Kavazi la Mwalimu la Mwalimu
Nyerere wakati wa ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa elimu ya juu katika maendeleo
ya Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam katikati ni Profesa Issa Shivji.
Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wa kushoto
akifungua kitambaa kuashiria kuzindua rasmi chapisho namba 4 la Kavazi la
mwalimu Nyerere wakati wa ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa elimu ya juu katika
maendeleo ya Afrika uliofanyika jijini Dar es salaam kushoto ni Profesa Issa
Shivji.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania,
Dkt. Mohammed Ghalib Bilal wa pili kushoto akifatilia kwa amakini mdahalo
wakati wa ufunguzi
wa Mhadhara wa Tatu wa elimu ya juu katika maendeleo ya Afrika uliofanyika
jijini Dar es salaam
Na
Ally Daud - MAELEZO
VIJANA wametakiwa kuienzi
na kuendelea kuitunza amani iliyoachwa na waasisi wa taifa ili kuijenga Tanzania yenye
amani na utulivu kwa mustakabali wa kizazi cha sasa na baadaye.
Hayo yamesemwa leo
Jijini Dar es Salaam na Waziri Mkuu Mstaafu Jaji Joseph Warioba wakati wa
ufunguzi wa Mhadhara wa Tatu wa Mwalimu Nyerere uliojadili maendeleo ya elimu
ya juu Afrika ulioambatana na ufunguzi wa hifadhi ya nyaraka ya Mwalimu Nyerere.
Jaji Warioba alisema kuwa vijana wanatakiwa kuenzi na
kuendeleza amani iliyoachwa na waasisi wetu kwa kuwa imejenga misingi bora katika kwa vizazi vya
Watanzania.
“Vijana ni nguvu kazi
ya taifa hivyo mnapaswa kuitunza na kuendeleza amani ambayo imeachwa na waasisi
wa taifa kwa maendeleo ya nchi yetu” amesema Jaji. Warioba.
Aidha Jaji Warioba
alisema kuwa vijana waache kutumia muda wao kuzungumzia na badala yake watumie
nguv na akili kufanya maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla ili kuijenga nchi.
Kwa mujibu wa Jaji
Warioba alisema kuwa vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele katika kuimarisha
umoja na mshikamano ili kuondokana na ubaguzi wa rangi, kabila, vyama vya siasa
na dini na kupigana na maadui watatu wa umasikini, ujinga na maradhi.
Mbali na hayo Jaji
Warioba aliwataka kuwa wanasiasa nchini kuwa msaada mkubwa wa wananchi badala
ya wananchi kugeuka msaada kwa wanasiasa.
No comments