TANZIA: TASWA YAOMBOLEZA KIFO CHA ELIZABERTH.
Chama Cha Waandishi wa Habari za
Michezo (TASWA),kimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba wa mwanachama
wake,Elizaberth Mayemba kilichotokea jana jioni huko nyumbani kwake
Tabata kwa Swai.
TASWA imestushwa na kuhuzunishwa sana kutokana na kifo hiki cha Elizaberth ambaye mchango wake katika tasnia ya habari za michezo bado ulikuwa unahitajika sana.
Waandishi wa Habari za michezo wataendelea kumkumbuka Elizaberth kutokana na ucheshi,kujituma na uwajibikaji katika kufanikisha kazi zake na kuwa mfano kwa waandishi chipukizi.
TASWA inatoa pole kwa familia ya marehemu, marafiki na waandishi wote wa habari na kuwatakia moyo wa subira katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mpendwa wetu.
Mwenyezi Mungu aipumzishe mahala pema peponi roho ya marehemu. TASWA ipo pamoja na familia ya marehemu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Juma Pinto
Mwemyekiti TASWA
Post Comment
No comments