Breaking News

WAZIRI MKUU WA INDIA AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA SIKU MBILI


Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi akiwasili uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere terminal I kwa kwa ndege ya shirika la Ndege la India kwa ziara ya siku mbili nchini kuanzia tarehe Julai 09-10, 2016
Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi akipunga mkono kusalimia wananchi waliojitokeza kumlaki mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere, Mhe. Modi atakuwa nchini kwa ziara ya siku mbili kuanzia tarehe Julai 09-10, 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akisalimiana na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda akisalimiana na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki akisalimiana na Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege.

Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana (wa kwanza kulia) akiwaongoza Waheshimiwa Mawaziri Wakuu wakati wa mapokezi


Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi akipunga mkono kuwasalimia wananchi waliojitokeza kumlaki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere


Baadhi ya vikundi vya burudani vikitumbuiza wakati wa mapokezi ya Waziri Mkuu wa India Mhe. Narendra Modi kwa ziara ya siku mbili nchini.

(Picha na Eleuteri Mangi)

No comments