WATENDAJI WA MKOA WA PWANI WATAKIWA KUWA WAWAZI KWA WAANDISHI WA HABARI PALE WANAPOTAKA KUPATA TAARIFA KUTOKA KWAO
Naibu
Waziri wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia
Wambura akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Mkoa Pwani
(hawapo pichani) alipofanya ziara yake ya kikazi leo mkoani kwa lengo la
kujua maendeleo ya kisekta kwa upande wa Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo.
Kaimu
Mkuu wa Mkoa Pwani Bw.Shangwe Twamala akitoa taarifa maendeleo ya
kisekta kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe.Anastazia Wambura (katikati) alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo
leo Mjini Kibaha.
Afisa
Tawala Wilaya ya Kibaha Bi. Sozy Mgate akieleza changamoto za sekta ya
michezo kwa Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo
Mhe.Anastazia Wambura (wa kwanza kushoto) alipofanya ziara ya kikazi
leo Mjini Kibaha kujionea maendeleo ya kisekta katika Mkoa huo.
Mwakilishi
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Mashariki Mhandisi
Christopher John akitoa ufafanuzi kuhusu kukosekana kwa usikivu wa
matangazo katika baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani kwa Naibu Waziri
Wizara ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura
(hayupo pichani) alipofanya ziara ya kikazi Mjini Kibaha,Mkoani Pwani
kwa lengo la kujua maendeleo ya kisekta katika mkoa huo.
Mbunge
wa Viti Maalum Pwani Mhe.Hawa Mchafu akimshukuru Naibu Waziri wa Wizara
ya Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (wapili
kushoto) kwa kutembelea Mkoa wa Pwani leo na kujionea changamoto za
kisekta zinazohusu Wizara yake.
Baadhi
ya Watendaji wa Ofisi ya Mkoa wa Pwani wakiwa katika picha ya pamoja na
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia
Wambura (watatu kushoto) alipofanya ziara ya kikazi Mjini Kibaha leo
kujionea maendeleo ya sekta kwa wizara yake, (wapili kushoto) ni Kaimu
Mkuu wa Mkoa Bw.Shangwe Twamala na (wapili kulia) Mbunge wa Viti Maalum
Mhe. Hawa Mchafu.
Baadhi
ya Maafisa Habari,Maafisa Michezo,Maafisa Utamaduni wa Mkoa wa Pwani
wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa
na Michezo Mhe.Anastazia Wambura (watatu kushoto) alipofanya ziara ya
kikazi leo Mjini Kihaba,Mkoani Pwani kujua maendeleo ya sekta kwa
wizara yake , (wapili kushoto) ni Kaimu Mkuu wa Mkoa Bw.Shangwe Twamala
na (wapili kulia) ni Mbunge wa Viti Maalum Pwani Mhe. Hawa Mchafu.
Na Anitha Jonas – MAELEZO
Watendaji
wa Mkoa wa Pwani watakiwa kuwa wawazi kwa waandishi wa habari pale
wanapotaka kupata taarifa kutoka kwao. Hayo yamesemwa leo Mjini Kibaha,
Mkoani Pwani na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.
Anastazia Wambura alipofanya ziara ya kikazi mkoani hapo kufuatilia
utekelezwaji wa maendeleo ya kisekta kwa wizara yake.
“Kwa
kuwapa ushirikiano wakutosha waandishi wa habari kutasaidia kuepuka
kuandikwa kwa habari zisizona taarifa kamili ambazo huleta mkanganyiko
kwa jamii na kuharibu taswira ya ofisi, hivyo ni vyema mshirikiane
nao”,alisema Naibu Waziri Wambura. Pamoja na hayo Mhe. Naibu Waziri
aliangiza kuwa katika bajeti ya mwaka 2016/2017 Kitengo cha Habari
kipewe kipaumbele na kitengewe bajeti itakayokidhi mahitaji pamoja na
kununuliwa vitendea kazi ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao kwa
urahisi ikiwa ni pamoja na kutangaza shughuli za maendeleo ya Mkoa.
Kwa
upande wa Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani Bw.Shangwe Twamala alisema mkoa
huo unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa Maafisa Michezo kwa baadhi ya
Wilaya pamoja na Maafisa Utamaduni ila suala hilo kwasasa
limeshawasilishwa kwa ngazi husika na wanalifanyia kazi. Pamoja na hayo
Kaimu wa Mkoa huyo aliendelea kusema Mkoa huo unakabiliwa pia na
changamoto ya usikivi wa matangazo ya Redio na Televisheni kwa baadhi ya
maeneo kama Rufiji,Mafia na mengineyo.
Naye
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya
Mashariki Bw.Bernard Haule alitoa ufafanuzi kuhusu suala la kukatwa kwa
matangazo katika chaneli zote pale malipo yanapoisha katika ving’amuzi
vya Azam na Zuku kwa kusema leseni zao ni tofauti na zile za Startimes
na Continental ambazo mbali na malipo ya kifurushi yanapokwisha wao bado
huonyesha chaneli tano za taifa bure ambazo ni ITV,Star Tv,Channel Ten,
EATV na TBC 1.
Pamoja
na hayo Mhe.Wambura aliagiza kuwa watendaji wahakikisheni wanatenga
maeneo ya viwanja vya michezo yasiyo na mgogoro kwani michezo ni ajira
na inasaidia vijana kujikwamua kiuchumi,hivyo ni vyema ipewe kipaumbele.
Halikadhalika
Naibu Waziri Wambura alitoa wito kwa wasanii Muziki wa Mkoa wa Pwani
kuiga mfano wa marehemu Baraka Mwishehe kwa kutunga nyimbo zenye maadili
na zenye kubeba ujumbe wa kuelimisha na kuburudisha jamii. Hata hivyo
Naibu waziri aliendelea kuwasisitiza watanzania wote kwa ujumla kuenzi
lugha ya Kiswahili kama yanavyofanya mataifa mengine duniani kuenzi
lugha zao mfano China.
No comments