Breaking News

Ummy Mwalimu:Wanaotaka Kujenga Viwanda Vya Dawa Tanzania Wahimizwa Kukidhi Vigezo


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wawekezaji wa ndani wanao taka kujenga viwanda vya dawa watakiwa kuhakikisha wanakidhi  vigezo vya uzalishaji wa dawa ili kuweza kuruhusiwa kufanya shughuli hiyo ya uzalishaji wa dawa.
Akizungumza mapema leo wakati  wa Uzinduzi wa maabara hamishika  zakudhibiti ubora na usalama wa dawa mapema leo jijini Dar es salaam alisema Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) kuakikisha inazingatia vigezo vya dawa sambamba na kikidhi viwango.
“Serikali itaendelea kuchukua jitihada za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa hasa dawa kwa kuimarisha mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa  mbao ulianza 2002 unaohusu uchunguzi wa Dawa muhimu za Kifua kikuu, Dawa za ARV, Dawa za Maleria pamoja na Viuwa sumu” alisema Mhe. Ummy.
Aidha  Mhe. Ummy amesisitiza athari za uwepo wa dawa zisizo na ubora katika jamii ikiwepo kuhathiri  uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kiujumla kutokana na kufanya manunuzi ya  Dawa zisizo na uwezo wa uwezo wa kutibu mwisho hupelekea usugu wa Dawa katika mwili.
Katika hatua nyingine mhe.Ummy ameipongeza Bodi, Uongozi na wafanyakazi  wa TFDA kwa utendaji  mzuri wa  kazi huku akiahidi kuendelea kushirikiana nao kwa ukaribu katika safari ya kumsaidia Raisi wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Magufuli.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA)  Hiiti Sillo alisema kuwa kutokana na kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia kuwabaini na kuwakamata wahalifu wanaofanya biashara hiyo ambayo inahathiri jamii na uchumi kiujumla.
“Mwaka 2005 wastani wa dawa bandia ulikuwa 3.7 wa dawa zilizokuwepo huku takwimu za 2017 imeshuka  kwa chini ya asilimia 1, mafanikio hayo yanatokana na ufuatiliaji wa umakini unaofanywa na taasisi hiyo” alisema Bw. Sillo.
Aidha Bw.Siilo aliongeza kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao TFDA imepanga kupeleka maabara hizo katika ofisi za kanda ambazo hazikuwa na huduma hiyo ikiwemo ofisi ya Tabora, Hospitali ya Mbeya na  Mtwara.


Amevitaja vituo vingine kuwa ni vituo vya Forodha Namanga, KIA mpakani, Silali (Tarime) na Mutukula (Kagera) bila kusahau Geita na Katavi, alisisitiza Bw. Sillo.

No comments