Benki Ya Pta Yabadili Jina, Sasa Kuitwa Benki Ya Tdb
Mkurugenzi wa Maswala ya Ndani na Uhusiano wa Wawekezaji wa benki ya
TDB, Mary Kamari akizungumza kuhusu PTA kubadili jina kuwa TDB na akielezea
mipango mbalimbali ambayo benki hiyo wanayo ili kuliwezesha baa la Afrika
kupata maendeleo makubwa.
Benki ya biashara na maendeleo mashariki na kusini
mwa afrika maarufu kama TPA imebadili rasmi jina la biashara Leo na kuanza
kutumia jina la TDB.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Maswala ya Ndani na Uhusiano wa
Wawekezaji wa benki ya TDB, Mary Kamari alisema kubadili jina kumekuja baada ya
miaka kadhaa ambapo ubora wa mali uliongezeka, upatikanaji wa faida, umepanda
na ubunifu unatumika ipasavyo, vitu vilivyotokana na mageuzi kadhaa ya muundo
mzima wa benki yanayolenga kuimarisha na kuifanya iwe ya kisasa zaidi.
“Tumeongeza kwa kaisi kikubwa
uwezi wetu wa kutosheleza mahitaji ya bidhaa na huduma zatu, kupitia mtandao
imara tuliojenga ukijumuisha waliowekeza kwetu na wafadhili wetu.
Wanahisa wetu wameongezeka kwa
zaidi ya asilimia 50 katika miaka ya karibuni zikiwemo taasisi kadhaa mpya za
uwekezaji na nchi wanachama,” alisema
Kimari.
Alisema benki
hiyo imejipanga kuendeleza utekelezaji wa miradi iliyopo kwenye sekta zenye
kupewa kipaumbele kama vile miundombinu, viwanda na biashara ya kilimo katika
nchi 21 ambazo inafanya shughuli zake kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
“Usanifu wa jina letu unaashiria kuibuka kwa nguvu
mpya na dhamira mpya katika kuimarisha biashara, Maendeleo ya uchumi pamoja na
ushirikiano wa kikanda katika kuakikisha kwa dhati kusukuma mbele mageuzi ya
kiuchumi na kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi” alisema
Kimari.
Katika miradi ya karibuni
tumechochea kasi yetu na kutoa mikopo katika biashara, ujasiriamali na
miundombinu na kuongeza mara tatu kwa fungu letu zima la mikopo katika
miaka mitano iliyopita. Tumechangia kwa kaisi kikubwa katika ukuaji wa sasa wa
uchumi na maendeleo ya miundombinu katika ukanda mzima.
Alisema
benki hiyo imetoa mikopo ili kufanikisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwa
ni pamoja na mradi 711 wa Kawe, Dar unaoendeshwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC), Fibre Optic Backbone Project wa nchini Burunndi, miradi ya nishati
endelevu ambayo inafanyika Kenya na Uganda na miradi ya viwanda vya simenti na
chuma katika nchi ya Congo DRC, Djibouti, Zambia, Rwanda, Ethiopia na Zimbabwe.
No comments