Ummy Mwalimu:Wanaotaka Kujenga Viwanda Vya Dawa Tanzania Wahimizwa Kukidhi Vigezo
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewataka Wawekezaji
wa ndani wanao taka kujenga viwanda vya dawa watakiwa kuhakikisha
wanakidhi vigezo vya uzalishaji wa dawa ili kuweza kuruhusiwa kufanya
shughuli hiyo ya uzalishaji wa dawa.
Akizungumza mapema leo wakati wa Uzinduzi wa maabara hamishika
zakudhibiti ubora na usalama wa dawa mapema leo jijini Dar es salaam alisema Mamlaka
ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) kuakikisha inazingatia vigezo vya dawa
sambamba na kikidhi viwango.
“Serikali itaendelea kuchukua jitihada
za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa hasa dawa kwa kuimarisha
mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa mbao ulianza 2002 unaohusu
uchunguzi wa Dawa muhimu za Kifua kikuu, Dawa za ARV, Dawa za Maleria pamoja na
Viuwa sumu” alisema Mhe. Ummy.
Aidha Mhe. Ummy amesisitiza
athari za uwepo wa dawa zisizo na ubora katika jamii ikiwepo kuhathiri
uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kiujumla kutokana na kufanya manunuzi
ya Dawa zisizo na uwezo wa uwezo wa kutibu mwisho hupelekea usugu wa Dawa
katika mwili.
Katika hatua nyingine mhe.Ummy
ameipongeza Bodi, Uongozi na wafanyakazi wa TFDA kwa utendaji mzuri
wa kazi huku akiahidi kuendelea kushirikiana nao kwa ukaribu katika
safari ya kumsaidia Raisi wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Magufuli.
Kwa upande wake Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo alisema
kuwa kutokana na kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia kuwabaini na
kuwakamata wahalifu wanaofanya biashara hiyo ambayo inahathiri jamii na uchumi
kiujumla.
“Mwaka 2005 wastani wa
dawa bandia ulikuwa 3.7 wa dawa zilizokuwepo huku takwimu za 2017
imeshuka kwa chini ya asilimia 1, mafanikio hayo yanatokana na
ufuatiliaji wa umakini unaofanywa na taasisi hiyo” alisema Bw. Sillo.
Aidha
Bw.Siilo aliongeza kuwa katika utekelezaji wa majukumu yao TFDA imepanga
kupeleka maabara hizo katika ofisi za kanda ambazo hazikuwa na huduma hiyo
ikiwemo ofisi ya Tabora, Hospitali ya Mbeya na Mtwara.
Amevitaja
vituo vingine kuwa ni vituo vya Forodha Namanga, KIA mpakani, Silali (Tarime)
na Mutukula (Kagera) bila kusahau Geita na Katavi, alisisitiza Bw. Sillo.
No comments