DOYO HASSAN DOYO NA MFAUME KHAMIS NDIO WAGOMBEA URAIS WA NLD BARA NA ZANZIBAR UCHAGUZI 2025
Mhe. Doyo Hassan Doyo kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bara na Mhe. Mfaume Khamis kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar mara baada ya kutangazwa kupeperusha bendera ya chama cha National League for Democracy (NLD) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
Mhe. Doyo Hassan Doyo kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bara kupitia chama cha National League for Democracy (NLD) akizungumza mara baada ya kupitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
Mfaume Khamis kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar akifafanua jambo mara baada ya kupitishwa na chama hicho kuwa mgombea wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
Doyo Hassan Doyo na Mfaume Khamis wakipiga kura
Dar es salaam - Chama cha National League for Democracy (NLD) kimemteua Mhe. Doyo Hassan Doyo kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania bara na Mhe. Mfaume Khamis kuwa Mgombea Urais wa Zanzibar katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
Akizungumza mara baada ya Uchaguzi huo Aprili 10, 2025 amesema Chama hiko wanapenda Taifa la Tanzania na hawapo tayari kujihusisha na chama chochote kutoshiriki Uchaguzi hivyo watashiriki zoezi hilo mpaka mwisho na. wanalinda tunu ya Amani iliyopo.
”Chama cha NLD tutaweka wagombea Nchi nzima hatuko tayari kususia Uchaguzi wala kuleta sababu zisizo kuwa na mashiko tuna Imani Sera zetu zitawafikia watanzania watatuchagua “. Alisema Doyo
Hata hivyo ameshukuru Chama chake kumuamini kuipeperusha kwa.kumpa dhamana ya kuwania Urais hivyo anaaihidi Watanzania wakimchagua atapambana na Mafisadi wala rushwa wote kwa kuweka adhabu ya viboko 24 kwa yeyeyote atakayebainika katika Serikali yake
Kwa upande wake Mgombea Urais Zanzibar Mfaume Khamisi Hassani ameshukuru kwa chama hiko kumuamini kwenda kupeperusha bendera ya NLD atahakikisha Wazanzibari wakimpatia Kura Serikali itakayoundwa itashughulika kutatua kero za wananchi zote zilizokuwa zikiwakabili .
Awali Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa Sisty Nyahoza ambaye lihudhuria kushuhudia Uchaguzi huo wa NLD amesisitiza kuwa chama chochote kilichosajiliwa kikatiba kinatakiwa kushiriki Uchaguzi hivyo amefurahishwa na mwenendo wa chama hiko
Doyo Hassan Doyo na Mfaume Khamis wakipongeza na baadhi ya wajumbe mara baada ya kupitishwa na chama hicho rasmu kuwa wagombea wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba mwaka huu.
Post Comment