Breaking News

RAIS DKT. SAMIA KINARA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA NCHINI - MSIGWA

Dar es salaam - Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema kwa kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, serikali imewekeza zaidi katika sekta ya afya nchini ambapo imeziwezesha huduma ya kuzalisha Oksijeni katika hospital ambayo awali ilikuwa ikinunuliwa nje kwa gharama kubwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juu ya mafanikio ya serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dokta Samia Suluhu Hassan kuhusu tangu kuingia madarakani amesema serikali imekuwa ikitoa kipaumbele zaidi katika sekta ya afya kwa kuongeza bajeti kwa lengo la kuhakikisha kuwa huduma za afya zinakuwa bora na za uhakika zaidi.

“Serikali imejenga mitambo ya kuzalisha hewa ya Oksijeni, huko nyuma tulikuwa tunanunua Oksijeni kutoka nje ya nchi, sasa hivi serikali imeamua kuwezesha hospitali kuzalisha Oksijeni yenyewe. Wote mtakumbuka kipindi cha Corona ilikuwa ni changamoto kubwa kwasababu watu walihitaji Oksijeni nyingi na upatikanaji wake ulikuwa ni wa gharama na kiukweli watu wengi walikuwa wanashindwa kumudu, sasa hivi tumeanza safari ya kuweka mitambo ya Oksijeni kwenye hospitali zetu na tayari kwa kipindi cha miaka minne tumefunga mitambo 21”, alisema Msigwa.

Akitoa takwimu ju ya halinya upatikanaji wa huduma za afya nchini amesema zahanati 677 vituo vya afya 425 na hospitali 100 zimepatiwa vifaa tiba huku vituo vya kutolea huduma za afya 129 vikiwa vimefungwa mfumo wa hewa tiba za Oksijeni.

Aidha, alisema katika kipindi cha miaka minne ya Samia Suluhu Hassan yamenunuliwa magari ya wagonjwa (Ambulance) 382, magari kwaajili ya madaktari 210, na yote yamesambazwa katika hospitali za wilaya na mikoa. Aidha amesema zimenunuliwa pikipiki 540 zinazofanya huduma za mkoba yaani kuwahudumia wananchi popote walipo.

No comments