Breaking News

BAKARI KIMWANGA MWENYEKITI MPYA DCP

Chama Cha Waandishi wa Habari, Mkoa wa Dar es salaam (DCP), kimemchagua Bakari Kimwanga kuwa Mwenyekiti wake mpya.

Bakari amefanikiwa kushinda nafasi hiyo kwa kura 68 akiwa ni mgombea pekee huku akipigiwa kura za hapana nane na zilizoharibika zikiwa tano.

Kwa ushindi huo Bakari anakuwa Mwenyekiti wa klabu hiyo ambayo ina wandishi wa Habari wa Dar es salaam wapatao 178.

Matokeo ya ushindi wa Bakari yametangazwa na Mwenyekiti wa Kamati huru ya uchaguzi, Wakili wa Kujitegemea, Raphael Awino, katika uchaguzi uliofanyika Februari 28, 2025, mjini Dar e salaam.

Mkutano huo wa uchaguzi ambao umehudhuriwa na wandishi wa Habari wa Dar es salaam wapatao 96 pia wamemchagua, Mary Geofrey, kuwa Makamu Mwenyekiti kwa kura 70 za ndiyo huku kura saba zikiwa za hapana na nne zikiharibika.

Uchaguzi huo umewapata wajumbe watano wa bodi na kura zao kwenye mabano ambao ni Selemani Jongo (69), Penina Malundo (62), Andrew Msechu (67) na Khamis Miraji (59) na Veronika Mrema (69), mgombea ambaye kura zake hazikutosha ni Selemani Msuya (43).

Uchaguzi huu umehitimisha uongozi wa Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Sam Kamalamo na Katibu wake, Fatma Jalala ambao walibaki na Mjumbe wa bodi Salehe Mohammed baada ya viongozi wengine kujiuzuru Kwa kile walichodai kutoridhishwa na mwenendo mbovu wa klabu.

Waliojihudhuru ni pamoja na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, Salome Gregory, Naibu Katibu Mkuu, Chalila Kibuda na Mweka hazina Patricia Kimelemeta.

Wajumbe wa bodi waliojihudhuru ni Shabani Matutu, Njumai Ngota, Taus Mbowe na Ibrahim Yamola. Uchaguzi wa DCP hufanyika kila baada ya miaka mitano.

No comments