Breaking News

DIWANI KIMJI AONGOZA KAMATI YA SIASA KUKAGUA MIRADI ULYA MAENDELEO

Na HERI SHAABAN - Diwani wa Kata ya Ilala Saady Kimji ,amefanya ziara ya Kamati ya Siasa kata ya Ilala leo February 25 /2025 katika kukagua miradi ya maendeleo ndani ya kata ya Ilala. 

Akizungumza katika ziara hiyo ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi Juni 2024 mpaka Desemba 2024 alisema Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, imefanya mambo makubwa katika kata ya Ilala kwa kuleta miradi mikubwa ya maendeleo. 

"Leo tulikuwa na ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kamati ya siasa ya kata ya Ilala pamoja na Kamati ya maendeleo kukagua miradi kamati ya siasa imejiridhisha miradi ya Dkt.Samia yote mizuri Ilala tunaembea kifua mbele kwa kazi kubwa aliyofanya Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na Mbunge wangu ambaye ni Naibu Spika Mussa Zungu " alisema Khimji. 

Katika ziara hiyo walitembelea shule ya msingi Mkoani, katika chumba cha Mfumo wa TEHAMA, Barabara za Kisasa zinazojengwa Ilala kwa kiwango cha lami pamoja na Ofisi ya Mtendaji wa kata ya Ilala pamoja na soko la kisasa Ilala Machinga Complex ambalo linatoa huduma masaa 24 kwa sasa.

Akizungumzia soko la kisasa la Machinga Complex alisema Serikali kwa sasa wameboresha soko hilo kwa ikiwemo kufunga taa kwa ajili ya maelekezo ya mkuu wa wilaya Edward Mpogolo na mkuu wa mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila ili huduma zifanyike muda wote

Akizungumzia sekta ya Elimu alisema katika utekelezaji wa Ilani shule ya msingi Mkoani kuna chumba maalum cha mfumo wa TEHAMA kwa ajili ya kufundishia, kwa upande wa miundombinu Barabara za kisasa Ilala zinaendelea kujengwa Ilala itakuwa ya kisasa sekta ya afya Serikali imejenga zahanati ya kisasa Ilala Bungoni ambayo inatoa huduma.

Diwani wa Viti Maalum Wanawake wilaya ya Ilala Aisha Kipini alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu na Diwani Saady Kimji kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri. 

Katibu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Ilala Devota Bantulaki na Kamati yake ya Utekelezaji wa kata wamelidhishwa na miradi ya maendeleo kazi kubwa imefanywa na Diwani wake Saady Kimji.

Katibu Devota Bantulaki alitumia fursa hiyo kupongeza Serikali kwa kuboresha soko la Machinga Complex ambalo linafanya kazi usiku na mchana. 

No comments