Breaking News

SERIKALI HAIWEZI KUAJILI WAHITIMU WOTE WA VYUO VIKUU - MSIGWA

Dar es salaam - Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, amesema Serikali itaajiri kulingana na uwezo wake wa kifedha na mahitaji, lakini haiwezi kutoa ajira kwa kila mhitimu wa chuo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkutano huo ulikuwa na lengo la kutoa ufafanuzi juu ya maendeleo na miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali.

Alisema serikali inatambua changamoto ya ajira kwa walimu na inafanya juhudi kuhakikisha nafasi zaidi zinapatikana, huku ikizingatia fursa zilizopo. Amefafanua kuwa suala la ajira sio kwa walimu pekee, bali hata tasnia nyingine kama uandishi wa habari, ambapo zaidi ya wanahabari 500 huhitimu kila mwaka bila ajira rasmi.

Kauli ya Msigwa imekuja kutokana na swali la waandishi wa habari kuhusu malalamiko ya Umoja wa Walimu Wasio na Ajira (NETO), ambao wamekuwa wakidai Serikali iwape kipaumbele katika ajira mpya.

"Serikali inaendelea kuangalia njia za kuongeza ajira kwa sekta mbalimbali kulingana na uwezo wake. Hatuwezi kuajiri kila mhitimu kwa wakati mmoja, lakini tunafanya juhudi kuhakikisha wale wenye uhitaji mkubwa wanapewa kipaumbele," Alisema Msigwa.

Kauli hii inakuja kufatia kujitokeza kundi la walimu wasio na ajira limeendelea kushinikiza Serikali kuongeza nafasi zaidi za ajira, huku Serikali ikihimiza vijana kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi nje ya sekta ya ajira za Serikali.
 

No comments